Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Biden kuimarisha uhusiano na chi za Ulaya

Rais wa Marekani, Joe Biden, anaanza wiki hii ziara yake rasmi ya kwanza nje ya nchi tangu aingie madarakani, ziara barani Ulaya wakati ambapo atashiriki mkutano wa kilele wa G7, NATO na Umoja wa Ulaya (EU) kabla ya mkutano na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin Juni 16 huko Geneva.

Rais wa Marekani anataka kutimiza ndoto yake ya kuirudisha nchi yake uwanja wa kimataifa
Rais wa Marekani anataka kutimiza ndoto yake ya kuirudisha nchi yake uwanja wa kimataifa REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mivutano ya pande nyingi ambayo ilionekana katika utawala wa mtangulizi wake Donald Trump, Rais Joe Biden kutoak chama cha Democratic atajaribu kurekebisha uhusiano na washirika wake na kuwahamasisha dhidi ya wapinzani wao wa pamoja, ikiwa ni pamoja na janga la COVID-19 au matarajio kutoka Moscow na Beijing.

Katika masuala hayo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya tabia nchi, viongozi wa nchi zilizostawi zaidi kiuchumi, G7, (Ujerumani, Canada, Marekani, Ufaransa, Italia, Japan na Uingereza ambayo inashikilia urais unaozunguka mwaka huu) wanataka kuonyesha kwamba nchi za Magharibi zinaweza kukabiliana na vitendo vya China na Urusi.

"Katika nyakati hizi za kutokuwa na uhakika, huku ulimwengu ukiwa bado unakabiliwa na janga la miaka mia moja, safari hii ni juu ya kuongeza upya juhudi au ahadi Marekani kwa washirika wetu na zile zinazotuunga mkono," almesema Joe Biden katika makala iliyochapishwa na Washington Post Jumamosi .

Kwa upande wake Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen, amesema makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa mwishoni mwa wiki hii na mawaziri wa fedha wa G7 juu ya kodi ya chini ya makampuni - ambayo inapaswa kuidhinishwa rasmi na viongozi wa G7 mwishoni mwa wiki - ni uthibitisho kwamba "ushirikiano wa pande nyingi unaweza kuzaa matunda".

Mkutano wa kilele wa G7, ambao utafanyika kuanzia Ijumaa hadi Jumapili, huko Cornwall, kusini magharibi mwa Uingereza, utakuwa mkipimo cha kwanza kwa mipano ya Joe Biden ya kurudisha Marekani kwenye uwanja wa kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.