Pata taarifa kuu
PALESTINA

ICC yadai kuwa na mamlaka ya kuchunguza kesi katika maeneo ya Palestina

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangaza kwamba inayo mamlaka ya kisheria ya kuchunguza kesi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Israel tangu vita vya mwaka 1967, hali ambayo inaweza kufungua njia ya uchunguzi wa uhalifu wa kivita.

ICC kuchunguza mlakosa ya kivita dhidi ya Wapalestina.
ICC kuchunguza mlakosa ya kivita dhidi ya Wapalestina. REUTERS/Raneen Sawafta
Matangazo ya kibiashara

ICC imeelezea katika taarifa kwamba "majaji wawili kati ya watatu wameamua kwamba mahakama hiyo ina mamlaka ya kisheria ya kuchunguza kesi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Israel tangu vita vya mwaka 1967.

Palestina ni taifa lililosaini mkataba na sheria ya Roma kuhusu kuundwa kwa ICC, imleongeza taarifa hiyo ya ICC.

Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka wa Mahakama hii ya Kimataifa iliyoundwa mnamo mwaka 2002 kushughulikia uhalifu mbaya zaidi uliofanywa ulimwenguni, alikuwa ameomba mahakama hiyoktoa maoni yake ya kisheria juu ya suala hili. Na hii ilikuja baada ya kutangaza mwezi Desemba 2019 kutaka kufungua uchunguzi kamili juu ya uwezekano wa "uhalifu wa kivita" - bila hata hivyo kutaja wahusika wa uhalifu huo - katika wilaya zinazokaliwa kimabavu na Israeli.

Bi Bensouda, ambaye ataondoka kwenye nafasi yake mwezi Juni mwaka huu, anataka ICC ifuatilie uchunguzi wa awali wa miaka mitano kufuatia vita vya mwaka 2014 katika Ukanda wa Gaza.

Israeli na Marekani, ambayo pia sio sehemu ya nchi zilizotia saini ya kuundwa kwa mahakama ya ICC, ililaani vikali mahakama hiyo wakati mwendesha mashtaka alipotoa ombi hili kwa uchunguzi kamili.

Wakati huo serikali ya Donald Trump ilichukua vikwazo dhidi ya Bi Bensouda mwezi Septemba 2020, ambaye naye alimuomba Joe Biden kumfutia vikwazo hivyo.

"Uamuzi huu (wa ICC) ni ushindi wa haki na ubinadamu, kwa maadili ya ukweli, haki na uhuru, na kwa damu ya wahanga na familia zao," amesema waziri mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh, ambaye alinukuliwa na shirika la habari la serikali nchini Palestina WAFA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.