Pata taarifa kuu
ITALIA

Wengi katika serikali watishiwa na chama cha Renzi

Rais wa serikali ya Italia, Giuseppe Conte, anakutana na serikali yake Jumanne wiki hii kujaribu kuzuia kasoro ya mmoja wa washirika wa muungano wake, ambao unaweza kuitumbukiza nchi hiyo kwenye mzozo mpya wa kisiasa katikati ya janga la Corona.

Waziri Mkuu wa Italia  Giuseppe Conte
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte Yara Nardi/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Italia ViVA, kinachoongozwa na mtangulizi wake Matteo Renzi, kinatishia kuondoa uungwaji wake mkono kwa serikali, ambayo kinashikilia nyadhifa mbili, kwa sababu tofauti, ikiwa ni pamoja na kuwekwa mashakani kwa mipango ya Giuseppe Conte kwa suala la mgawanyo wa mabilioni euro zilizoahidiwa Roma na mpango wa wa kusaidia uchumi wa Umoja wa Ulaya.

Baraza la mawaziri limepangwa kufanyika saa 3:30 usiku na ikiwa chama cha Italia ViVA kitathibitisha upinzani wake, Giuseppe Conte atapoteza wingi katika Bunge.

Mazungumzo yaliyofanywa katika siku za hivi karibuni yameshindwa kupata muafaka wa pamoja na viongozi wa vyama vingi vimemwonya Matteo Renzi dhidi ya hatari za kupasuka kwa muungano huo.

"Ninaamini kuwa itakuwa kosa kubwa la kisiasa ambalo litaiathiri Italia na ambayo Waitaliano hawataelewa," Nicola Zingaretti, katibu wa kitaifa wa Chama cha Democratic (PD), amekiambia kituo cha televisheni cha Sky Italia.

Vyama vya muungano vinaweza kujaribu kujadili mpango mpya ambao unaweza kusababisha mabadiliko makubwa ya serikali, pamoja au la na Giuseppe Conte kwenye uongozi. Lakini Vito Crimi, kiongozi wa chama cha 5 Star Movement (M5S), chama kikuu cha wengi, amekataa wazo hili.

"Ikiwa Renzi ana hatia kwa kuwaondoa mawaziri wake, hakuwezi kukawa na serikali nyingine pamoja naye na chama cha Italia VIVA. Kuna mipaka kwa kila kitu," Vito Crimi ameliambia shirika la habari la ANSA.

Chanzo katika washirika wa karibu wa Giuseppe Conte kimethibitisha kuwa rais wa serikali hakutaka kujaribu kufikia mkataba mpya wa muungano ikiwa mawaziri wa Italia Viva wataondoka serikalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.