Pata taarifa kuu
UTURUKI-SIASA-USALAMA-EU

Mediterania Mashariki: EU yapanga vikwazo vipya dhidi ya Uturuki

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameamua kuandaa vikwazo dhidi ya maafisa kadhaa wa Uturuki katika muktadha wa mzozo na Ugiriki na Cyprus juu ya utaftaji wa nishati, wakibaini kwamba hatua kali zinaweza kuchukuliwa mwezi wa Machi.

Rais wa Uturuki  Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Adem ALTAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Umoja wa Ulaya pia wamekubaliana kwa taarifa ya pamoja ya kuidhinisha, pamoja na mambo mengine, raia wa Uturuki na makampuni zinazohusika katika shughuli za uchimbaji wa mafuta katika eneo linalozozaniwa la Mashariki mwa Mediterania.

Ugiriki imeelezea kufadhaika kwake kwa kusita kwa Umoja wa Ulaya kwa kulenga uchumi wa Uturuki, wakati Ujerumani, Italia na Uhispania zilitaka kutoa muda zaidi kwa masuala ya kidiplomasia.

Uturuki, mwanachama wa NATO na ambayo inatafuta kujiunga na Umoja wa Ulaya, inapingana na Ugiriki na Cyprus eneo la Mashariki mwa Mediterania, na kuhusu haki zao uchimbaji wa rasilimali zinazowezekana kutoka eneo hilo.

Wakati huo huo, Marekani inapanga kuiwekea Uturuki vikwazo baada ya kupata mifumo ya ulinzi wa anga S-400 mwaka jana kutoka Urusi.

Uturuki imeendeleza mzozo wake na Ugiriki kwa kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la Mashariki mwa bahari ya Mediterania linalozozaniwa kati ya Ankara na Athens.

Hii ilifuatia hatua ya Ugiriki kupeleka wanajeshi kwenye kisiwa kilicho karibu na Uturuki. Uendelezaji huo wa mzozo kati ya mahasimu hao wa kihistoria unachochewa na ugunduzi wa gesi asili katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.