Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA

Ufaransa kuanza kulegeza masharti ya watu kutembea

Serikali ya Ufaransa sasa inasema uvaaji wa barakoa katika maeneo ya umma ni lazima katika vita dhidi ya maambukizi ya Corona, wakati huu inapojiandaa kutangaza kulegeza masharti ya watu kutembea tarehe 11 mwezi Mei.

Kiongozi wa chama cha France insoumise Jean-Luc-Mélenchon alipinga mpango wa kulegeza masharti ya watu kutembea uliowasilishwa na Waziri Mkuu Edouard Philippe (picha ya kumbukumbu)
Kiongozi wa chama cha France insoumise Jean-Luc-Mélenchon alipinga mpango wa kulegeza masharti ya watu kutembea uliowasilishwa na Waziri Mkuu Edouard Philippe (picha ya kumbukumbu) Ludovic Marin / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mpango wa kulengeza masharti ya watu kutembea umepitishwa bungeni nchini Ufaransa licha ya kukosolewa na upinzani kuhusu mfumo uliopitishwa na serikali.

Mpango huo uliowasilishwa bungeni na Waziri Mkuu Edouard Philippe umepitishwa na wabunge 368, wabunge 100 waliupinga baada ya zaidi ya masaa matano ya mjadala.

Waziri Mkuu Edouard Philippe amesema pia shule zitaanza kufunguliwa hatua kwa hatua, huku ligi kuu ya soka na michezo nyingine ikiahirishwa hadi mwezi Septemba mwaka huu.

Watu zaidi ya 23,000 wamepoteza maisha na wengine 129,000 wakiambukizwa virusi vya Corona kwa mujibu wa Wizara ya afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.