Pata taarifa kuu
DUNIA-G7-UCHUMI-USALAMA

G7: Mkutano wa kilele wa Biarritz wamalizika kwa "tamko" la pamoja

Mkutano wa kilele wa G7 uliokuwa ukiendelea katika mji wa Biarritz ulimalizika Jumatatu jioni wiki hii kwa "tamko la pamoja lenye ukurasa mmoja kuhusu biashara na migogoro ya kimataifa.

Rais Emmanuel Macron aonyesha taarifa ya mwisho iliyopitishwa na kundi la G7, Biarritz.
Rais Emmanuel Macron aonyesha taarifa ya mwisho iliyopitishwa na kundi la G7, Biarritz. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

"Ukurasa huu niliiandika mwenyewe, baada ya mlolongo wa majadiliano, haukuandikwa hapo awali, ulisambazwa kwa viongozi na kupitishwa na viongozi," Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari. Ufaransa ndio inaongoza mwaka huu Kundi la mataifa 7 yaliostawi zaidi kiviwanda (G7).

"Kutakuwa na ufuatiliaji, tutaunda tume huru ya ufuatiliaji kuhusu ahadi tulizozitoa" katika taarifa hii ambayo suala la tabia nchi halipo, Emmanuel Macron ameongeza.

♦ Kuhusu Ukraine

"Ufaransa na Ujerumani zitaandaa mkutano wa kilele huko Normandie katika wiki zijazo ili kupata matokeo thabiti. "

Kwa mujibu wa Emmanuel Macron, mambo yote yako sawa kwa kufanyika mkutano huo "muhimu" wa wakuu wa nchi na serikali katika muundo wa "Normandy" (Ufaransa, Ukraine, Urusi, Ujerumani) mnamo mwezi Septemba kujaribu kusuluhisha mzozo wa Ukraine.

♦ Kihusu biashara kaytika ngazi ya kimataifa

"G7 imejitolea kusimamia biashara huru katika ngazi ya kimataifa, biashara yenye usawa na utulivu wa uchumi wa dunia. G7 inawataka mawaziri wa kifedha kufuatilia hali ya uchumi wa dunia. "

"Kwa hiyo, G7 inataka kufanya mabadiliko ya kina kwenye shirika la kimataifa la biashara (WTO) ili iweze kuwa na ufanisi zaidi katika ulinzi wa mali, kumaliza haraka mizozona kutokomeza tabia zisizo endana na biashara. "

"G7 imeahidi kupata mkataba mnamo mwaka 2020 ili kurahisisha vizuizi vya kisheria na ushuru wa kisasa katika mfumo wa OECD. "

♦ Kuhusu Iran

"Tunmeafikiana kikamilifu malengo mawili: kuhakikisha kwamba Iran isiwezi kupata silaha za nyuklia; na kuunga mkono mchakato wa amani na utulivu katika ukanda wa Mashariki ya Kati. "

♦ Juu ya Libya

"Tunaunga mkono usitishwaji mapigano nchini Libya hali ambayo inaweza itaruhusu mkataba wa kudumu wa usitishwaji mapigano. Tunaamini kuwa suluhisho la kisiasa pekee ndilo litahakikisha utulivu wa Libya."

"Tunatoa wito kwa mkutano wa kimataifa ulioandaliwa vizuri utakaowashirikisha wadau wote na wahusika wakuu katika mgogoro wa Libya kutoka Ukanda huo. "

"Kwa hiyo, tunaunga mkono kazi ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuanzisha mkutano wa unaowaleta pamoja wadau wote nchini Libya. "

♦ Kuhusu Hong Kong

"G7 inathibitisha kuwapo na umuhimu wa Azimio la mwaka 1984 lililotolewa na China na Uingereza kuhusu Hong Kong na wametoa wito wa kuepukana na vurugu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.