Pata taarifa kuu
UFARANSA-VANUATU-HAKI

Balozi wa Ufaransa Vanuatu akabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia

Balozi wa Ufaransa Vanuatu Robby Judes anashutumiwa kuwanyanyasa kimapenzi baadhi ya wanawake katika eneo hilo. Robby Judes, aliyeteuliwa miezi minne iliyopita kwenye nafasi hiyo, anakabiliwa na mashitaka mawili katika ofisi ya mwendesha mashitaka ya Noumea huko New Caledonia.

Port Vila, mji mkuu wa Vanuatu, Novemba 2006 (pichaya kumbukumbu).
Port Vila, mji mkuu wa Vanuatu, Novemba 2006 (pichaya kumbukumbu). Auscape/UIG via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya Nje ya Ufaransa, Quai d'Orsay, imemuitisha nyumbani jijini Paris kwenda kumsikiliza. RFI imeweza kuzungumza na mmoja wa waathirika wa kitendo hicho.

Mkasa huo ulitokea wakati wa chakula cha jioni cha kati ya viongozi wa makampuni na wawakilishi wa vyama vya siasa, siku nane zilizopita huko Nouméa. Lakini mikutano hii ya kwanza ya kiuchumi kati ya New Caledonia na Vanuatu imeingiliwa na kasoro kulingana na ushuhuda wa Chérifa Linossier, kiongozi wa Shirikisho la makampuni madogo madogo ya wastani.

"Balozi Robby Judes alipita nyuma yangu, akagusa makalio yangu. Wakati huo, nilidhani alikosa nafasi na hivyo kunisukuma kidogo ili aweze kukaa, wala sikufikiria chochote. Lakini baadaye alirudi na wakati huo, alinigusa mgongoni na kwenye makalio, akaniambia kwamba anataka kuniona tena, "amesema Cherifa Linossier."

Baada ya kuguswa na jambo hilo, Cherifa Linossier tangu siku mbili silizopita, anakutana na wanachama wenzake wa mashirika mengine yaliwakilishwa katika mikutano hiyo. Na kwa sasa amekuta kuwa kuna wanawake wengine saba ambao walinyanyaswa kijinsia kutukanawa na balozi Robby Judes katika miezi ya hivi karibuni. "Kunaweza kuwa na wanawake wengi waliofanyiwa kitendo kama hicho, "amesema Cherifa Linossier.

"Ni vitendo ambavyo havikubaliki na ambavyo vinatakiwa kukemewa au kuchukuliwa hatua," Cherifa Linossier ameongeza. Kwa hiyo natumaini kwamba wanawake ambao halisita kuongelea kitendo hicho wanaweza kutoa ushahidi na wasiwi na hofu ya kueleza kilichotokea. "

Mashitaka mawili tayari yamewasilishwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa mara moja imejibu. Balozi Robby Judes ameitishwa nyumbani jini Paris. Anatarajiwa kusikilizwa Jumatano wiki hii na Mkurugenzi Mkuu wa Utawala kwenye wizara hiyo. Hatima yake itajadiliwa, kuhusiana na ofisi ya wairi wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian.

"Kesi hiyo imechukuliwa kwa uzito kwa nia ya kuzingatia umuhimu wa ukweli na madai ya kutokuwa na hatia," chanzo kutoka Quai d'Orsay kimeiambia RFI. RFI imekua ikijaribu kuzungumza na balozi Robby Judes, mpaka sasa haijaweza kumpata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.