Pata taarifa kuu
UJERUMANI-USALAMA

Ujerumani yawashikili Wasyria sita kwa tuhuma za kupanga mashambulizi

Polisi ya Ujerumani imewakamata Wasyria sita wanaoshutumiwa kupanga mashambulizi na silaha au mabomu kwa niaba ya kundi la Islamic State, ofisi ya mashtaka ya Frankfurt imetangaza.

Polisi ya Frankfurt inaendelea na operesheni ya kuwasaka wapiganaji wa IS.
Polisi ya Frankfurt inaendelea na operesheni ya kuwasaka wapiganaji wa IS. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa hao, walio na umri kati ya miaka 20 na 28, walikamatwa wakati wa msako katika miji ya Kassel, Hanover, Essen na Leipzig, Ofisi ya mashitaka imeongeza katika taarifa yake.

Polisi 500 walishiriki katika operesheni hiyo iliofanyika katika nymba nane.

Watuhumiwa wanne waliwasili Ujerumani mwezi Desemba 2014 na wawili walifika mwaka uliofuata. Wote sita walikuwa wameomba hifadhi ya ukimbizi. Ofisi ya mwendesha mashitaka haijasema kama maombi yao yalikubaliwa.

Wasyria sita wanashukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Islamic State, " ofisi ya mashitaka imebaini.

"Watuhumiwa hao pia wanahukumiwa kupanga shambulizi dhidi ya raia nchini Ujerumani kwa kutumia silaha au mabomu," ofisi ya mashtaka imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.