Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Raia wa Catalonia watishia kutotii serikali kuu ya Uhispania

Siku chache baada ya serikali ya Uhispania kutangaza kuwa inatazamia kudhibiti taasisi zote za Catalonia na zote hizo ziwe chini ya mamlaka ya Madrid, serikali ya jimbo la Catalonia imesema "hivyo ni vitisho vya Uhispania" na kamwe hawatokubali kuwa chini ya mamlaka ya serikali kuu.

Carles Puigdemont wakati wa hotuba yake Oktoba 21,2017.
Carles Puigdemont wakati wa hotuba yake Oktoba 21,2017. Ruben Moreno Garcia/Generalitat de Catalunya/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mvutano unaendelea nchini Uhispania kuhusu kujitenga kwa jimbo la Catalonia. Theluthi tatu ya wakazi wa Catalonia, au nusu yao, wanaweza kuingia mitaani na kupinga uamuzi wa serikali kuu ya Uhispania.

Chama cha mrengo wa kushoto CUP, mshirika wa wanaharakati wanotetea uhuru wa Catalonia kimetoa wito wa kutotii serikali kuu ya Uhispania.

Karibu nusu ya maafisa wa Zima Moto wanasema hawatatambua mamlaka yoyote kuliko "rais wa Catalonia na bunge lao".

Makundi ya wanafunzi wa vyuo Vikuu yameitisha maandamano siku ya Alhamisi mjini Barcelona, lakini bado kuna matumaini kwamba mazungumzo yatafanyika kuhusumvutano huu kati ya serikali ya Catalonia na serikali kuu ya Uhspania.

Bunge la Catalonia linatazamia kukutana leo Jumanne kujadili hatua hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.