Pata taarifa kuu
UFARANSA-MACRON-AFRIKA-SIASA

Viongozi wa Afrika waendelea kumpongeza Emmanuel Macron kwa ushindi wake

Salamu na pongezi kutoka viongozi wa nchi za Morocco, Senegal, Mali, Guinea, Niger, kwa ushindi wa Emmanuel Macron, rais mpya wa Ufaransa, zimeendelea kumiminika. Emmanuel Macron si maarufu barani Afrika.

Emmanuel Macron, akisherehekea ushindi wake katika mji wa Louvre, Mei, 7 2017.
Emmanuel Macron, akisherehekea ushindi wake katika mji wa Louvre, Mei, 7 2017. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron, mgombea bado kijana katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, alipata ushindi kwa kumuangusha mpinzani wake mkuu Marine Le Pen.

■ Nchini Cote d' Ivoire, Alassane Ouattara ametumia mtandao wa Twitter kwa kumpongeza Emmanuel Macron na alimhakikishia kuwa yuko "tayari kutoa ushirikiano wake kwa ajili ya kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya Cote d'Ivoire na Ufaransa."

■ Kuchaguliwa kwa Emmanuel Macron kama rais wa Ufaransa umewafurahisha wananchi wa Senegal, nchi ambayo ina uhusiano wa nguvu na Ufaransa. Macky Sall, rais wa nchi hiyo amemwandikia barua rais mpya wa Ufaransa akisema, "Napendelea tuendelee kuimarisha mapoja nanyi uhusiano wa kipekee kati ya nchi zetu mbili." marais hawa wawili wanajua vizuri na wako tayari kushirikiana kwa pamoja.

■ Mohamed wa 6, Mfalme Morocco amempongeza Emmanuel Macron, akisema kwamba kuchaguliwa kwake ni "taji" kwa siasa yake. "kiongozi huyo, kwa niaba ya wananchi wa Morocco, na kwake jina lake binafsi ametoa salamu na pongezi kwa Emmanuel Macron kwa ushindi wake akimtakia mafanikio mema katika majukumu hayo ya uongopzi wa nchi ya Ufaransa.

■ Rais wa Guinea Alpha Condé amesema kuwa "anaamini kwamba mahusiano ya ushirikiano kati ya Ufaransa na Guinea vizuri baada ya kuchaguliwa kwa Emmanuel Macron."

■ Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita Amesema kufurahishwa na ushindi wa Emmanuel Macron. Ufaransa ilitoa ushiriki wake nchini Mali tangu mwaka 2012 kwa ikiwa ni pamoja na operesheni ya kijeshi ya Serval, Barkhane katika kupambana dhidi ya ugaidi.

■ Nchini Niger, Issa Garba, mwanaharakati wavyama vya kiraia, amekaribisha ushindi wa mgombea wa En Marche !. Kwa mujibu wa Bw Garba, rais kijana ambaye alishinda bila msaada wa chama cha jadi, lazima awe mfano na kielelezo kwa vijana wote wa Afrika.

■ Nchi Chad, ambapo Rais Idriss Deby alimpokea mgombea wa chama ca National Front Marine Le Pen, amesema matokeo haya ni furaha kwake. Saleh Kebzabo, kiongozi wa upinzani nchini Chad, amesema kuwa ana matumaini kuwa rais mpya Ufaransa atakuwa na uwezo wa kumaliza mitandao iliopo kati ya Ufaransa na Afrika.

■ Nchini Jamguri ya Kidemokrasia ya Congo , upinzani unaamini kwamba mkakati wa mpasuko uliomfikisha Emmanuel Macron madarakani nchini Ufaransa ni sawa na ule unaoendeshwa na vijana wa DRC wanaodai demokrasia zaidi. Hayo ni maoni ya Pierre Lumbi, rais wa kundi la vyama 7 (G7), vilivyojiondoa katika muungano wa vyama vinavyounga mkono serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.