Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAUEL VALLS-UGAIDI

Bunge lapigia kura kuongezwa muda wa miezi 6 kwa hali ya tahadhari

Baada ya shambulizi la mjini Nice, kuongezwa muda wa miezi sita kwa hali ya tahadhari uliyoombwa na Serikali ya Ufaransa, hatimaye umepitishwa na Wabunge usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano hii.

Mbele ya Wabunge, Waziri Mkuu Manuel Valls ameelezea umuhimu wa kuongzwa muda wa hali ya tahadhari dhidi tishio la kigaidi. Ombi hilo la Serikali hatimaye limepitishwa kwa mara ya nne Julai 19, 2016.
Mbele ya Wabunge, Waziri Mkuu Manuel Valls ameelezea umuhimu wa kuongzwa muda wa hali ya tahadhari dhidi tishio la kigaidi. Ombi hilo la Serikali hatimaye limepitishwa kwa mara ya nne Julai 19, 2016. FRANCOIS GUILLOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mjadala mkubwa uliyofanyika usiku kwa muda wa masaa 8, ulipelekea kuibuka kwa mvutano kati ya Waziri Mkuu Manuel Valls na wawakilishi wa upinzani.

Kama ilivyokua ikidaiwa na upande mmoja wa vyama vya mrengo wa kulia, baada ya mjadala huo, Wabunge waliidhinisha kuongezwa muda wa miezi sita kwa hali ya tahadhari, hadi mwisho wa mwezi wa Januari 2017. Rais François Hollande aliambiwa wazi. Awali, serikali ilipanga kuongeza muda wa miezi mitatu kwa hali ya tahadhari.

Kwa upande wa vyama vya mrengo wa kushoto, mashambulizi ya mjini Nice yameonyesha haja ya kuchukua hatua kali dhidi ya ugaidi, kama alivyosema Eric Ciotti: "Wananchi wetu wanajua kwamba vita havishindi kwa silaha za zisiyotumiwa. "

Kupitisha sheria maalum, kubadilisha Katiba, baadhi ya wanasiasa wa vyama vya mrengo wa kulia wako tayari, lakini waziri mkuu kutka chama cha Kisoshalisti amejibu hapana. Amewatolea wito kwa mara nyingine tena kudumisha umoja, wakati ambapo shambulizi la mjini Nice lilipelekea Serikali kukusolewa vikali na wapinzani.

Katika hotuba yake, Manuel Valls kwa mara nyingine tena ameonya kuwa huenda ikakumbwa na "mashambulizi mengine" na "mauaji ya watu wasio na hatia."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.