Pata taarifa kuu
UFARANSA

Washukiwa watano wa tukio la ugaidi nchini Ufaransa wakamatwa

Polisi nchini Ufaransa wanasema watu watano wanaoshukiwa kupanga tukio la mtu aliyewagonga watu mjini Nice na kusababisha vifo vya watu 84 siku ya Alhamisi usiku, wanazuiliwa.

Eneo la kuwakumbuka watu waliopoteza maisha mjini Nice nchini Ufaransa
Eneo la kuwakumbuka watu waliopoteza maisha mjini Nice nchini Ufaransa REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Le Monde limeripoti kuwa, polisi walifanikiwa kuwakamata washukiwa hao siku ya Jumamosi huku wawili wakitiwa mbaroni siku ya Ijumaa.

Aidha, imebainika wazi sasa kuwa Mohamed Lahouaiej-Bouhlel mwenye asili ya Tunisia, ndiye aliyeliendesha Lori hilo na kutekeleza mauaji hayo kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Kundi la Islamic State limedai kuwa dereva wa lori hilo alikuwa ni mfuasi wao.

Serikali nchini humo imetangaza kuongeza muda wa hali ya hatari nchini humo kwa  miezi mitatu zaidi kwa sababu za kiusalama.

Rais Francois Hollande aliyetaja tukio hilo kama la kigaidi, leo Jumamosi anaongoza kikao cha dharura kuhusu kilichotokea siku ya Alhamisi usiku mjini Nice.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.