Pata taarifa kuu
UNGEREZA-MAREKANI-OBAMA

Obama aiomba Uingereza kutojiondoa katika EU

Rais wa Marekani Barrack Obama yuko katika ziara ya siku tatu nchini Uingereza. Mapema hivi leo amekutana na Malkia Elizabeth wa pili ambaye jana alitimiza miaka 90 ya kuzaliwa na kupata pamoja chakula cha mchana.

Rais Obama amemtembelea Malkia Elizabeth II, mjini Windsor Aprili 22, 2016.
Rais Obama amemtembelea Malkia Elizabeth II, mjini Windsor Aprili 22, 2016. REUTERS/John Stillwell/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais Obama amenukuliwa katika Gazeti la Daily Telegraph akiitaka Uingereza kusalia katika Umoja wa Ulaya na hata kusema kuwa nchi hiyo inaweza kukabiliana ipasavyo na makundi kama Islamic State ikiwa ndani ya Umoja huo.

"Nasema kwa moyo mkunjufu kwa mtu kama rafiki, kwamba matokeo ya uamuzi wako ni wa maslahi ya kina kwa Marekani," ameandika rais wa Marekani. "Umoja wa Ulaya haupunguza ushawishi wa Uingereza, bali unaongeza," Obama amehakikisha. "Kwa hiyo Marekani na dunia wana haja ya ushawishi wako mkubwa kuendelea, ikiwa ni pamoja na katika Umoja wa Ulaya," Obama amesema, na hivyo kujikubalisha kusaidia katika kampeni inayoendelea ya kura ya maoni.

Lakini je, rais Obama anaweza kuwashawishi wapiga kura nchini Uingereza kupiga kura ya ndio wakati wa zoezi hilo mwezi Juni ? Hili ni swali kila mtu amekua akijiuliza.

Zaidi ya Wabunge mia moja kutoka chaa cha conservative ambao wanataka Uingereza ijiondoe katika Umoja wa Ulaya pia wamemuandika Balozi wa Marekani mjini London wakipinga mwenendo wa Rais Obama wa"kuingilia kati" masuala ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.