Pata taarifa kuu
UHISPANIA-SIASA

Uhispania: PODEMOS yasimamisha mazungumzo na PSOE

Chama cha mrengo wa kushoto cha PODEMOS kimetangaza Jumatao hii kwamba kimesimamisha mazungumzo na chama cha Kisoshalisti cha PSOE kwa lengo la kuunda serikali ya muungano nchini Uhispania.

Kiongozi namba mbili wa chama cha PODEMOS, Inigo Errejon, Desemba 20, 2015, Madrid.
Kiongozi namba mbili wa chama cha PODEMOS, Inigo Errejon, Desemba 20, 2015, Madrid. GERARD JULIEN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Chama hiki kinakinyooshea kidole cha lawama chama cha PSOE baada ya makubaliano ya chama hicho na kile cha CIUDADANOS juu ya mpango ulifutiliwa mbali na Podemos.

Makubaliano hayo "yanazuia uwezekano wa kuunda serikali yenye wajumbe wengi na mabadiliko," amesema katika mkutano na waandishi wa habari Inigo Errejon, namba mbili wa cham cha PODEMOS, ambapo uungwaji mkono si muhimu kwa chama cha Kisoshalisti kwa ajili ya uzinduzi wa Bunge wakati wa mjadala uliopangwa kuanzia Machi 1.

Baada ya makubaliano hayo, "Tunashtumiwa kushindwa kumtawaza Pedro Sanchez," amesema Bw Errejon.

Kwa upande wake chama cha PODEMOS kimesema kwamba, chama cha PSOE kimevutiwa na itikadi ya chama cha CIUDADANOS, inazohusiana hasa na sheria za kazi, na mpango wao hauhakikishi ulinzi zaidi kwa wafanyakazi, wakati ambapo mageuzi ya soko la ajira yalioendeshwa na chama cha mrengo wa kulia mwaka 2012 tayari yalipunguza kwa kiasi kikubwa haki zao.

Mkataba uliosainiwa Jumatano na chama cha PSOE na CIUDADANOS, ambao unahusisha uungwaji mkono wa chama cha mrengo wa kati kwenye uzinduzi wa kiongozi kutoka chama cha Kisoshalisti, "unatutuhimu sera za kiuchumi ambazo tunataka kuziondoa ," amesema kiongozi wa Ujumbe wa chama cha PODEMOS unaoshiriki mazungumzo hayo.

Uchaguzi wa wabunge wa Desemba 20 ulisababisha mazingira ya kisiasa yanagawanyika nchini Uhispania, pamoja na vyama vikuu vinne, ambapo hakuna hata kimoja ambacho kina wabunge wa kutosha kwa kuongoza peke yake: wabunge kutoka chama cha Conservative ndio wanaongoza kwa wingi, wakifuatiwa na chama cha Kisoshalisti cha PSOE, kisha chama cha msimamo mkali cha mrengo wa kushoto PODEMOS na chama cha CIUDADANOS kinachukua na fasi ya nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.