Pata taarifa kuu
UTURUKI-SHAMBULIO-USALAMA

Ankara: watu 28 wauawa katika shambulio la bomu

Watu wasiopungua ishirini na nane wameuawa na wengine zaidi ya sitini wamejeruhiwa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari, shambulio ambalo limetokea katika mji wa Ankara Jumatano hii jioni.

Maafisa wa Idara ya huduma za dharura wakikabiliana na moto uliosababishwa na mlipuko wa gari ya kijeshi katika mji wa Ankara, Februari 17, 2016.
Maafisa wa Idara ya huduma za dharura wakikabiliana na moto uliosababishwa na mlipuko wa gari ya kijeshi katika mji wa Ankara, Februari 17, 2016. REUTERS/Ihlas News Agency
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi shambulio hili limekua limelenga magari yaliokua yamebea askari. taarifa hii imethibitishwa na mkuu wa mkoa mji mkuu wa Uturuki, Ankara, Mehmet Ali Kiliçlar.

Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amefuta ziara yake ya mjini Brussels.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Uturukila Hürriyet Daily News, mlipuko ihuo umetokea karibu na majengo ya kijeshi. Msemaji wa polisi katika mji mkuu wa Uturuki ametoa taarifa kwamba mlipuko uliosikika ni wa bomu lililokua limetegwa ndani ya gari, bila kutoa maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa runinga ya NTV, mlipuko ulitokea wakati ambapo gari ndogo lililokua likibeba askari lilipopita katika eneo la Kizilay.

Magari mengi ya wagonjwa yametumwa haraka eneo la tukio, runinga za Uturuki zimeongeza, huku zikibaini moshi mkubwa umekua ukionekana juu ya eneo la tukio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.