Pata taarifa kuu
UFARANSA-SARKOZY-BYGMALION

Ufaransa: Nicolas Sarkozy afanyiwa uchunguzi

L’ancien président Nicolas Sarkozy a été mis en examen ce mardi 16 février pour financement illégal de sa campagne présidentielle de 2012, dans le cadre de l’affaire Bygmalion.

Uchunguzi huu ni pigo jipya kubwa kwa Nicolas Sarkozy.
Uchunguzi huu ni pigo jipya kubwa kwa Nicolas Sarkozy. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Ufaransa, ambaye anapanga kushindana katika kambi yake katika msimu ujao ili aweze kurudi madarakani mwaka 2017, amewasili kwa gari ndogo saa 2:40 asubuhi katika eneo maarufu la kibiashara kunakopatikana Mahakama ya mji wa Paris.

Nicolas Sarkozy tayari alishtakiwa kwa kashfa ya rushwa na kosa la ushawishi katika kesi ya udukuzi, ambapo anatuhumiwa kuwa alijaribu, mapema mwaka 2014, kupata taarifa kamili iliokua siri katika utaratibu wa sheria kutoka hakimu mwandamizi. Katika kesi hiyo, majaji wa uchunguzi walijulisha mwisho wa uchunguzi wao na kuna hatari kiongozi wa chama cha Republican kutumwa katika mahakama ya uhalifu.

Utafiti wa Bygmalion, jina la kampuni iliyoandaa mikutano ya kampeni zake, unaanza kuhusu mfumo wa kina wa mfumo wa risiti za uongo ili kuficha kiwango rasmi ambacho hakingelipaswi kupitishwa katika matumizi ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2012, sawa na Euro milioni 22.5. Bili hizo za uongo zilitolewa kwa minajili ya kudanganya kuwa chama cha UMP, ambacho kilibadilishwa jina na kuitwa Republican, kuwa kilitumia Euro milioni 18.5 katika kampeni zake. Hata hivyo, Baraza la Katiba lilifutilia mbali kiwango hicho.

Maafisa kadhaa wa kampuni ya Bygmalion, mhasibu wake pamoja na Jérôme Lavrilleux, walitambua kuwepo kwa udanganyifu katika risiti za uongo, lakini hakuna mtu yeyote alimhusisha Nicolas Sarkozy kuwa aliamua matumizi au kufahamu uwepo wa pesa hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.