Pata taarifa kuu
TABIA NCHI-UFARANSA-MAKABILIANO

Ufunguzi wa mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya Hali ya hewa umefungulia Jumpili hii Novemba 29, huku washiriki wakisalia kimya dakika moja kwa kuwakumbuka waathirika wa mashambulizi ya jijini Paris.

Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa umezinduliwa  Jumapili Novemba 29, 2015.
Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa umezinduliwa Jumapili Novemba 29, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa imetoa wito kwa ajili ya "maelewano" wakati wa ufunguzi wa majadiliano jijini Paris siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa marais na viongozi wa serikali Jumatatu Novemba 30.

"Usimamizi wa wakati wetu utakuwa muhimu" na "ingelipaswa kila siku tuwa na maendeleo", Laurent Fabius, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na Rais wa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (COP21), amesema.

Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utaanza rasmi Jumatatu Novemba 30 jijini Paris nchini Ufaransa.

Viongozi zaidi ya mia moja kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huu unaokuja siku kadhaa baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi jijini Paris.

Usalama umeimarishwa jijini Paris kuhakikisha kuwa wale wote wanaohudhuria mkutano huo utakaomalizika tarehe 11 Desemba na kuwakutanisha wajumbe zaidi ya elfu 40 mbali na viongozi wa dunia, wanakuwa salama.

Lengo kuu la mkutano huu ni kuona namna dunia inavyoweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na hasa ongezeko la joto duniani.

Rais wa Marekani Barrack Obama ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mkutano huo.

Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu.
Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu. Reuters/Mike Hutchings

Kwa upande wake Askofu mkuu nchini Afrika Kusini na msindi wa tuzo ya Amani ya Nobel Desmond Tutu ameonya viongozi wa dunia kutokea kwa hatari kubwa ya "mgogoro wa kiuchumi na uhamiaji" iwapo mkutano huu unaoanza Jumatatu Novemba 30 utashindwa.

Mara ya mwisho mkutano kama huu kufanyika ilikuwa mwaka 2009 jijini Copenhagen nchini Denmark.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.