Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UFARANSA-UJASUSI

BND ya Ujerumani yampeleleza Laurent Fabius

Idara ya Ujasusi ya Ujerumani (BND) inakisiwa kuwa ilimpeleleza mwanadiplomasia wa Ujerumani pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa nchi zilio naushirika na Ujerumani, ikiwa ni pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, kituo cha redio ya Ujerumani RBB Inforadio kimethibitisha.

Makao Makuu ya Idara ya Ujasusi ya Ujerumani (BND) mjini Berlin (BND).
Makao Makuu ya Idara ya Ujasusi ya Ujerumani (BND) mjini Berlin (BND). Reuters/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Haikuwezekana kupata maoni rasmi juu ya taarifa hiyo.

Nchini Malta, ambapo anaandamana na Rais François Hollande katika mkutano wa kilele wa Ulaya juu ya mgogoro wa uhamiaji, Laurent Fabius alisikika akisema kuwa huenda akaomba maelezo zaidi kutoka Ujerumani. "Tutajitenga na Wajerumani. wakati tutathibitishiwa hali hiyo, inasikitisha sana", Fabius amesema kwenye runinga ya iTELE.

Bila kufafanua utambulisho wa vyanzo vyake, RBB (Radio Berlin Brandenburg) imeripoti Jumatano kwamba BND ilimchunguza na kumpeleleza mwanadiplomasia wa Ujerumani, Hansjörg Haber, ambaye aliongoza ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya nchini Georgia kati ya mwaka 2008 na kisha mwaka 2011alikuwa akifanya kazi jijini Brussels. Kwa sasa ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Uturuki.

Katiba ya Ujerumani inakataza upelelezi kwa raia wa Ujerumani.

Miongoni mwa wanaolengwa na BND, ni Laurent Fabius na wajumbe wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague, wa Shirika la Afya Duniani, wa FBI ya Marekani na makampuni ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.