Pata taarifa kuu
TABIA NCHI-UFARANSA

Tabia nchi: mawaziri kutoka nchi 60 wakutana Paris

Mawaziri kutoka nchi sitini wamekutana jijini Paris Jumapili Novemba 8 ili kuharakisha mazungumzo juu ya mkataba wa kimataifa ili kupiga vita ongezeko la joto duniani, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa baadaye wa COP21, Laurent Fabius.

Alama ya Mkutano kuhusu tabia nchi (COP21) mjini Paris.
Alama ya Mkutano kuhusu tabia nchi (COP21) mjini Paris. AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Novemba 30, siku ya ufunguzi wa mkutano kuhusu tabia nchi (COP21), zaidi ya marais na viongozi wa serikali mia moja , ikiwa ni pamoja na marais wa Marekani na China watahudhuria mkutano huo, Laurent Fabius ametangaza.

" Ni maisha hata katika dunia yetu ambayo iko hatarini, kuna uharaka kabisa ", Waziri wa mamabo ya nje wa Ufaransa amesema. Laurent Fabius ametembelea eneo kubwa kunakojengwa jengo la mikutano katika mji wa Bourget, karibu na mji wa Paris, hasa ukumbi utakao wapokea watu 2,000.

Ili kuepuka kushindwa, kama katika mkutano wa Copenhagen mwaka 2009, kumeamuliwa viongozi waletwe katika siku ya kwanza ya mkutano huo, ambao utatamatika Desemba 11.

" Kabla ya mkutano huo wa mwisho wa mwaka, mkutano huu wa mawaziri unaotangulizwa utaendelea hadi Jumanne Novemba 10, na utatafutia njia ya maelewano kuhusu idadi inayowezekana ya masuali ", Laurent Fabius amesema, akifungua mkutano huo Jumapili hii alasiri.

Baada ya kikao cha pamoja cha Jumapili hii, Jumatatu mawaziri watakutana katika vikundi kwa mada zifuatazo: haki, nia, Fedha za baada ya mwaka 2020 na vitendo kabla ya mwaka 2020. Laurent Fabius, hatimaye atawasilisha hitimisho la shughuli za Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.