Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki yapata mafanikio lakini kuna vizuizi

Ugiriki na wafadhili wake wa kimataifa wamefikia katika hatua ya kuridhisha kwenye mazungumzo yao. Hayo yameshuhudiwa katika mikutano ya wiki hii iliyokua ikiendeshwa kwa kasi kwa lengo la kufikia makubaliano kuhusu madeni ya Ugiriki.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras na rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, Juni 3 mwaka 2015, Brussels.
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras na rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, Juni 3 mwaka 2015, Brussels. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano mdogo uliyofanyika katika mji wa Berlin Ujerumani kati ya Ufaransa, Ujerumani, Benki ya ECB, Shirika la kimataifa la Fedha (IMF) na Tume ya Ulaya, Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, aliwasili Jumatano jioni wiki hii katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, kwa ajili ya mazungumzo zaidi na washirika wake wa Ulaya.

Tume ya Ulaya ilionya kuwa mkutano hakuwa na lengo la kufikia matokeo ya mwisho, lakini waangalizi wote wanasubiri uamzi wa mwisho baada ya miezi mitatu ya mazungumzo ambayo yamekuwa yamechelewa kuanza. Mbali na Alexis Tsipras, upande wafadhili waliokuwepo katika mkutano huo ni pamoja na rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker na rais wa wa nchi zinazochangia sarafu ya Euro, Jeroen Dijsselbloem, wakiambatana na wawakilishi wa Shirika la Fedha Duniani na Benki Kuu ya Ulaya. Majadiliano yalidumu zaidi ya masaa manne hadi baada ya usiku wa manane.

Nchi za Ulaya zimewasilisha kwa Alexis Tsipras mapendekezo kutoka mkutano mdogo uliyofanyika jijini Berlin kuepuka kusema kuwa ilikuwa ni kuchukua au kuacha, hata kama mageuzi ya soko la ajira na pensheni bado yameendelea kuwatia wasiwasi wakati ambapo imekua ni vigumu wasiwasi huo kupita mbele ya macho ya serikali Ugiriki.

Hata hivyo, hakuna budi kuamini kwamba maendeleo halisi yameshuhudiwa tangu Waziri mkuu Ugiriki Alexis Tsipras alibaini katika usiku wa Jumatano kuamkia leo Alhamisi kwamba yuko karibu sana na makubaliano, hasa juu ya malengo ya fedha. Ulaya kwa kiasi kikubwa imepunguza masharti kuhusu kiwango ambacho Ugiriki inapaswa kufikia katika suala la ziada ya bajeti na Alexis Tsipras inaonekana yuko tayari kujiunga na hayo, hata kama malengo hayo yalikua yameonekana kuwa yamepita kiasi kabla ya mkutano.

Hata hivyo Alexis Tsipras hakukubaliana na pendekezo la kuongeza VAT kwa umeme au kupunguza faida ya kijamii na pensheni, lakini amesema kwamba hapakuwa na kauli ya mwisho kwa wakati wowote ule. Mazungumzo yamepangwa kuanza katika siku zijazo, huku kukiwa na matumaini kwani rais wa nchi zinazochangiya sarafu ya Euro mwenyewe ameyataja mazungumzo hayo kuwa yamekua yenye faida kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.