Pata taarifa kuu
UINZA-IS-UGAIDI-USALAMA

IS: “Jihadi John”, muaji wa mateka hatimaye ajulikana

“ jihadi John”, mpiganaji huyu wa kundi la wapigajai wa Dola la Kiislamu ambaye alikua akionekana katika video nyingi za mauaji ya mateka, inasadikiwa kuwa anaitwa Mohammed Emwazi.

Muuaji wa James Foley na mateka wengine huenda ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Koweit aitwaye Mohammed Emwazi.
Muuaji wa James Foley na mateka wengine huenda ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Koweit aitwaye Mohammed Emwazi. REUTERS/Social Media Website via REUTERS T
Matangazo ya kibiashara

“ jihadi John” ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Koweit, na anatambuliwa na idara za usalama, lakini ndugu zake ndio wamemtambua na kupelekea jarida la Washington Post kumfichua.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, mjini London, Muriel Delcroix, mtu huyo aliitwa kwa jina la “Jihadi John” na kundi la mateka. Mtu huyo alihusika kwa kuwakata vichwa mateka kutoka nchi za magharibi na wanajeshi wa Syria.

Kwa mujibu wa washington Post, Mohammed Emwazi, mwenye asili ya Koweit, aliwasili nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka sita, na alikua akiishi magharibi mwa London. Emwazi ni kutoka familia yenye maisha ya kati, na alihitimu chuo kikuu, na baadae aliufundisha katika shule mbalimbali kabla ya kuwa mwenye itikadi kali za kidini na baadae kujiunga na mwanaharakati anaeshirikiana na Al Shabab nchini Somalia.

Mohammed Emwazi alijulikana na idara za usalama za Uingereza, ambazo zilimhoji mwaka 2006, baada ya kufukuzwa Tanzania. Idara ya ujasusi inasadikiwa kuwa ilijaribu kumsajili bila maafaniko, lakini mtu huyo alikua chini ya ulinzi mkali wa viongozi hadi alipopotea, na kushukiwa kuwa huenda alisafiri Syria.

Serikali ya Uingereza haijathibitisha jina la mwanaharakati huyo wa kundi la Dola la wapiganaji wa Kiislamu, na ilikataa kutaja jina la mtu huyo kwa kuhofia kuhatarisha usalama wa mateka wanaoshikiliwa na Wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu (IS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.