Pata taarifa kuu
JORDANI

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lamuidhinisha mwanamfalme wa Jordan, Zeid al-Hussein

Kwa mara ya kwanza kwenye historia, baraza la Umoja wa mataifa limemuidhinisha bila kupingwa mwanamfalme wa Jordan, Zeid al-Hussein kuwa mkuu mpya wa tume ya haki za binadamu ya umoja huo akichukua nafasinya Navi Pillay raia wa Afrika kusini.

Mfalme Abdallah II, akizungumza na Bunge jipya la Jordani mnamo february 10 mwaka wa 2013 mjini Amman.
Mfalme Abdallah II, akizungumza na Bunge jipya la Jordani mnamo february 10 mwaka wa 2013 mjini Amman. REUTERS/Ali Jarekji
Matangazo ya kibiashara

Zeid al-Hussein anakuwa muislamu na kiongozi wa kwanza kutoka jumuiya ya nchi za kiarabu kuongoza tume ya haki za binadamu, jukumu ambalo atalianza rasmi september mosi mwaka huu.

Katibu mkuu Ban amemteua al-Hussein kuchukua nafasi hiyo akimueleza kuwa miongoni mwa watu waliochangia kwa sehemu kubwa kuongoza harakati za kutetea haki za binadamu kwenye eneo la mashariki ya kati na dunia kwa ujumla.

Zeid al-Hussein ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa kwenye kuanzishwa kwa mahakama ya kimataufa ya uhalifu wa kivita ya ICC iliyoko mjini the hague Uholanzi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.