Pata taarifa kuu
Uingereza

Ndoto za Manchester United zaota mbawa, yachapwa 1-0 na Everton Ligi Kuu ya Uingereza

Ndoto za timu ya Manchester United jana ziliota mbawa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya klabu ya Everton.Kwa matokeo hayo Man U imeanza vibaya msimu na kocha wa timu hiyo Sir Alex Fugerson ana kibarua kigumu cha kuhakikisha anakisuka kikosi chake. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Manchester United jana ilishuka ndimbani ikiwa ni mchezo wake wa kwanza katika ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Baclays dhidi ya timu ya Everton huku ikitarajiwa kumuanzisha mchezaji wake mpya Roben Van Persie.

Mchezaji Van Persie hii leo anatarajiwa kuonyesha makeke yake ya ufungaji na pengine kukata kiu ya mashabiki wa Manchester United ambao wana matumaini makubwa na mchezaji huyo aliyeihama klabu ya Arsenal.

Pia Man U inaelekea kumchezesha mchezaji wake Nemanja Vidic ambaye ameikosa kwa muda mrefu timu yake kutokana na majeraha.

Hata hivyo Manchester United huenda ikawakosa wachezaji wake wanne kutokana na kuwa majeraha na hivyo kutokumudu kucheza hali ambayo inawatia wasiwasi mashabiki.

Wachezaji hao ambao wanatarajiwa kutokuonekana katika kikosi hicho ni pamoja na Rio Ferdinand aliyeumia wakati wa mazoezi, Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans.

Kwa upande wake Everton inatarajiwa kuwakosa wachezaji wake Marouane Fellaini na Darron Gibson ambao pia wanasumbuliwa na majeruhi.

Hiyo jana katika mfululizo wa ligi Kuu ya Uingereza iliyoanza kutimua vumbi jumamosi wiki iliyopita Chelsea waliibamiza Wigan bao 2-0 wakati timu ya Manchester City waliibamiza Southampton bao 3-2.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.