Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Uongozi wakubali Didier Drogba kuondoka Chelsea

Klabu ya Chelsea tayari imethibitisha kwamba mshambuliaji wake Didier Drogba ataondoka katika klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa mwezi Juni.Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Chelsea Ron Goley amempamba nyota huyo kwamba anaondoka katika kipindi ambacho yuko juu kutokana na matokeo ya mchezo wa fainali za klabu bingwa barani Ulaya na kuongeza kuwa Drogba atabaki kuwa sehemu ya familia ya klabu hiyo.

REUTERS/Olivia Harris
Matangazo ya kibiashara

Awali wachezaji wa klabu ya Chelsea ambayo ilitwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya, wamesema mchezaji Didier Drogba hatakuwa tena katika kikosi hicho kwa sababu hakupenda kuendelea kuwa katika benchi akishuhudia wachezaji wengine wakicheza mpira uwanjani.

Mchezaji huyo amesema kuwa asingependa kuwa hivyo hususan wakati huu klabu hiyo ya chelsea ikijipanga kusuka kikosi kipya.

Drogba alikaririwa na jarida la France Football kuwa aliwaambia wachezaji wenzake kuwa hawataendelea kuwa pamoja katika timu hiyo ingawaje yeye mwenyewe bado hajaweka wazi kuwa atatua wapi baada ya kuondoka.

Drogba amesema kuwa japokuwa yeye mwenyewe hakupenda kuondoka namna hiyo lakini hakua na njia ya kuendelea kubaki katika klabu hiyo ya Uingereza uamuzi ambao ulikua mgumu kuuchukua.

Pamoja na Grogba kutokuwa wazi kuna tetesi ambazo zinamhusisha mchezaji huyo na hatua ya kujiunga na klabu ya Shanghai Shenhuan ya China ambayo anachezea mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Nicolas Anelka huku akishika jukumu jingine la ukocha wa timu hiyo.

Mashabiki wa Chelsea pamoja na wachezaji wenzake wamekuwa wakishinikiza mchezaji huyo apewe mkataba mpya kutokana na uwezo wake katika kuisaidia timu hiyo na mashabiki wanalazimika kusubiri mpaka kitendawili hicho kiteguliwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.