Pata taarifa kuu
UHOLANZI

Goran Hadzich kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini Serbia apandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza

Kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Serbia, Goran Hadzich ambaye anakabiliwa na mashataka ya uhalifu wa kivita katika mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa hii leo amepandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza kusomewa mashtaka.

Goran Hadzich
Goran Hadzich Online
Matangazo ya kibiashara

Akiwa amevalia suti nyeusi, Hadzich alijitambulisha kwa kujiamini mbele ya majaji wanaosikiliza kesi yake huku akishindwa kukanusha wala kukubali mashtaka yanayo mkabili.

Hatua hiyo ilifanya majaji kuingilia kati na kuhoji ambapo wakili anayemtetea Hadzich, Vladimir Petrovic aliwaambia majaji kuwa mteja wake hii leo hatoweza kuzungumzia chochote kuhusiana na mashtaka yanayomkabili mpaka wakati mwingine.

Hadzich alikamatwa juma lililopita kaskazini mwa Serbia baada ya miaka saba ya kukimbia huku akitafutwa na polisi na mahakama ya Umoja wa Mataifa kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Mtuhumiwa huyo anatajwa kuhusika moja kwa moja na vita na nchi ya Croatia miaka ya 1990 ambapo aliamuru mauaji ya maelfu ya raia wa serbia na Croatia wakati wa vita hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.