Pata taarifa kuu
Australia

Safari za ndege zaahirishwa nchini Australia kuafuatia wingu la jivu la Volcano la nchini Chile

Maelfu ya abiria wanao safiri kwa ndege wameendelea kutaabika, kwa siku ya tatu leo, nchini Australia, kufuatia wingu la jivu lililotokana na volcano iliyolipuka nchini Chile na kusababisha kuahirishwa kwa safari za anga.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya ndege ya Qantas na Jetstar, yameanza safari zake za kuingia na kutoka jijini Melbourne, lakini yameahirisha safari za kisiwani Tasmania, Adelaide na halikadhalika nchini New Zealand kwa siku ya leo.

Aidha, shirika la ndege la Tiger Airways, limeahirisha huduma zake kati ya Adelaide, Melbourne na Perth.

Mlipuko wa volcano ya Puyehue, iliyofika mpaka katika milima ya Andes, imerusha jivu hatari na hivyo kuathiri sekta ya usafiri, kwa kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu kutokea kwa wingu la volcano nchini Iceland, na kuathiri bara la Ulaya mwaka jana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.