Kombe la Dunia la Soka 2023: Morocco yapata ushindi wa kihistoria dhidi ya Korea Kusini
Baada ya kushindwa dhidi ya Ujerumani (6-0), Morocco, ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake, imepata ushindi wa kihistoria dhidi ya Korea Kusini kwa kuifunga bao 1-0 huko Adelaide, nchini Australia.
Imechapishwa:
Morocco, haikufikiriwa kuwa itafanya vizuri katika mashindano hayo, imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano hii ya Kombe la Dunia la Wanawake, dhidi ya Korea Kusini (1-0), Jumapili Julai 30, huko Adelaide, kwa bao la kichwa lililowekwa kimyani na Ibtissam Jraidi dakika ya 6 ya mchezo.
Wachezaji hao wanaonolewa soka na kocha Reynald Pedros, waliochapwa na Ujerumani (6-0) walipoingia kwenye kinyang'anyiro hicho, wamesalia kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kwa hatua ya 16 bora, kabla ya kumenyana na Colombia siku ya mwisho ya kundi H, Alhamisi, Agosti 3.
(Pamoja na AFP)