Pata taarifa kuu

Taaluma ya Zlatan Ibrahimovic

NAIROBI – Mchezaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 41, na hivyo kuhitimisha taaluma yake katika mchezo huo.

 Zlatan Ibrahimovic, aliyekuwa mchezaji wa AC Milan
Zlatan Ibrahimovic, aliyekuwa mchezaji wa AC Milan REUTERS - ALBERTO LINGRIA
Matangazo ya kibiashara

Ibrahimovic alikuwa tayari ametangaza kuondoka katika klabu hiyo ya Italia kabala ya kufanya hivyo rasimi siku ya Jumapili.

"Ninaaga mpira lakini sio kukuaga wewe," raia huyo wa Sweden aliuambia umati wa San Siro baada ya mchezo wa mwisho wa msimu wa Jumapili.

Alifunga mabao 511 kwa vilabu vikiwemo Paris St-Germain, Manchester United na AC na Inter Milan, akishinda mataji ya ligi katika nchi nne.

Ibrahimovic alirejea AC Milan kwa mara ya pili mapema 2020, baada ya kushinda nao taji mwaka 2011, na kuwasaidia kushinda taji tena msimu uliopita.

Zlatan Ibrahimovic amestaafu kutoka soka
Zlatan Ibrahimovic amestaafu kutoka soka © AC MILAN

Alicheza mara nne pekee na alianza mechi moja kwa upande wa Serie A msimu huu - na alifunga bao moja - kufuatia mfululizo wa majeraha, na mkataba wake ulikuwa unamalizika mwezi huu.

"Kuna hisia nyingi sana kwangu kwa sasa. Forza Milan na kwaheri," Ibrahimovic mwenye hisia alisema, akizuia machozi.

“Mara ya kwanza nilipokuja hapa ulinipa furaha, mara ya pili ulinipa mapenzi.

"Ulinikaribisha kwa mikono miwili, umenifanya nijisikie niko nyumbani, nitakuwa Milanista maisha yangu yote."

Zlatan Ibrahimovic amekuwa na taaluma yenye mafanikio katika soka
Zlatan Ibrahimovic amekuwa na taaluma yenye mafanikio katika soka © AC MILAN

Ibrahimovic alishinda mataji 34 - ikiwa ni pamoja na mataji 14 ya ligi - katika taaluma iliyoanza katika karne iliyopita, na aliteuliwa kuwania Ballon d'Or mara 11.

Mshambulizi huyo pia alistaafu kama mfungaji bora wa muda wote wa Uswidi akiwa na mabao 62 ya kimataifa katika mechi 122.

Aliondoka katika timu ya taifa baada ya Euro 2016 lakini akarejea 2021 kwa kampeni yao ya kufuzu Kombe la Dunia ambayo haikufaulu.

"Nilikuwa naogopa waandishi wa habari walipouliza kuhusu mustakabali wangu, lakini sasa naweza kukubali, niko tayari," aliwaambia waandishi baada ya tangazo lake.

"Nimekuwa nikifanya hivi maisha yangu yote. Kandanda ilinifanya kuwa mtu. Iliniwezesha kujua watu ambao singewahi kuwafahamu. Nimesafiri duniani kutokana na soka. Yote ni shukrani kwa soka."

Mchezaji huyo ameagwa na mashabiki, wachezaji wenzake na uongozi wa AC Milan
Mchezaji huyo ameagwa na mashabiki, wachezaji wenzake na uongozi wa AC Milan © AC MILAN

                                            Taaluma yenye mafanikio

Ibrahimovic alianza maisha yake ya soka akiwa na klabu ya Malmo FF mwaka 1999 kabla ya kuhamia Ajax mwaka 2001 kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo alishinda mataji matatu ya ligi.

Alihalia Juventus mwaka wa 2004, ambapo alishinda mataji mawili ya ligi, ambayo baadaye yalipokonywa klabu hiyo kutokana na kashfa ya Calciopoli.

Hata hivyo, Msweden huyo alishinda mataji mengine matatu ya Serie A akiwa na klabu yake iliyofuata, Inter Milan, kabla ya kuhamia Barcelona mwaka 2009.

Zlatan Ibrahimovic aliwahi kuichezea Barcelona
Zlatan Ibrahimovic aliwahi kuichezea Barcelona (Photo: Reuters)

Ibrahimovic alitumia msimu mmoja pekee katika klabu hiyo ya Catalan, akishinda taji la La Liga kabla ya kupelekwa kwa mkopo AC Milan, uhamisho ambao ulifanywa kuwa wa kudumu mwaka 2011.

Mwaka mmoja baadaye, hata hivyo, na Ibrahimovic alikuwa kwenye harakati tena, akisaini Paris St-Germain, ambapo alifunga mabao 113 katika mechi 122 za ligi na kushinda mataji manne ya Ligue 1.

Zlatan Ibrahimovic wakati akiichezea PSG
Zlatan Ibrahimovic wakati akiichezea PSG AFP/Archives

Mnamo Julai 2016, alisajiliwa na Manchester United kwa kipindi cha miaka miwili na kilabu hiyo ya Uingereza ilimfanya kushinda Kombe la Ligi na Ligi ya Europa.

Ibrahimovic alisajiliwa na klabu ya LA Galaxy ya MLS mwaka 2018, akitumia misimu miwili huko California kabla ya kurejea AC Milan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.