Pata taarifa kuu

Riadha: Okagbare afungiwa kwa miaka 10 kwa matumizi ya dawa za kusisimua misuli

Mwanariadha wa Nigeria Blessing Okagbare amesimamishwa kwa muda wa miaka kumi kwa ukiukaji wa sheria nyingi za kupinga matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini, Kitengo cha Uadilifu cha Riadha (AIU) kimetangaza: "Miaka mitano kwa uwepo na matumizi ya dawa nyingi zilizopigwa marufuku na miaka mitano kwa kukataa kushirikiana na uchunguzi wa AIU. " 

Blessing Okagbare, mwanariadha  wa Nigeria katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2021.
Blessing Okagbare, mwanariadha wa Nigeria katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2021. AFP - GIUSEPPE CACACE
Matangazo ya kibiashara

Blessing Okagbare ambaye alikuwa mshindi wa medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, katika mashindano ya dunia ya mwaka 2013, na kututnukiwa katika mashindano mengi ya Afrika, alifukuzwa katikati ya Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2021 baada ya kuthibitishwa kuwa ana chembe chembe za madawa hayo siku chache kabla.

Je, huu ndio mwisho wa kazi ya Blessing Okagbare? Raia huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 33 amesimamishwa kwa muda wa miaka 10 kwa ukiukaji mwingi wa sheria dhidi ya utumiaji wa dawa za kusisimua misuli, Kitengo cha Uadilifu cha Riadha (AIU) kimetangaza mnamo Februari 18, 2022. Adhabu ya kipekee ambayo Kitengo cha Uadilifu cha Riadha kinabaii kwamba: " Miaka mitano kwa uwepo na matumizi ya dawa nyingi zilizopigwa marufuku na miaka mitano kwa kukataa kushirikiana na uchunguzi wa AIU. "

Mwanariadha huyu, mshindi wa medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, katika mashindano ya Dunia ya mwaka 2013 na kutwaa taji katika mashindano mengi ya Afrika, alisimamishwa kwa muda katikati ya Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2021, siku chache baada ya kuthibitishwa kuwa na chembe chembe za madawa ya kusisimua mwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.