Pata taarifa kuu
SOKA-TP MAZEMBE

Bejaia Mouloudia na TP Mazembe kumenyana katika fainali

Klabu ya Algeria Bejaia Mouloudia imefuzu kucheza fainali ya Kombe la shirikisho, Jumapili tarehe 25 Septemba katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, baada ya kutoka sare ya kufungana.

TP Mazembe wamefuzu katika fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kutoka sare (0-0) dhidi ya Etoile du Sahel siku ya Jumapili 25 Septemba.
TP Mazembe wamefuzu katika fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kutoka sare (0-0) dhidi ya Etoile du Sahel siku ya Jumapili 25 Septemba. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Bejaia Mouloudia ilipata ushindi huo katika dakika za mwisho, baada ya mchezai Faouzi Rahal kufunga bao la kusawazisha.

Katika mechi ya awaliya nusu fainali, Algeria ilitoka sare na Morocco ya kutofungana (0-0).

Mouloudia Bejaia inajiandaa kucheza fainali dhidi ya klabu ya DR Congo ya TP Mazembe, ambao waliwaaibisha Etoile Sportive du Sahel, klabu ya Tunisia.

TP Mazembe walitoka sare ya kutofungana (0-0) na Etoile Sportive du Sahel siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba.

klabu hizi mbili zilitoka sare katika mechi ya kwanza ya kufungana 1-1 mjini Tunis.

Mechi za awali na marudiano za fainali zitapigwa mwishoni mwa mwezi Oktoba na mapema mwezi Novemba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.