Pata taarifa kuu
CAF-RWANDA-SOKA

Almany Kabele ziarani Kigali

Makamu wa wa pili wa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF Almany Kabele, amewasili jijini Kigali nchini Rwanda. Kabele amesema amefurahishwa na maandalizi ya nchi hiyo kuwa wenyeji wa michuano ya mataifa ya Afrika baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN mapema mwakani.

Michuano ya CHAN itaanza kuchezwa tarehe 16 Januari hadi tarehe 7 mwezi wa Februari mwaka 2016 katika jiji la Kigali, mjini Huye na Rubavu.
Michuano ya CHAN itaanza kuchezwa tarehe 16 Januari hadi tarehe 7 mwezi wa Februari mwaka 2016 katika jiji la Kigali, mjini Huye na Rubavu. YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo ya CHAN itaanza kuchezwa tarehe 16 Januari hadi tarehe 7 mwezi wa Februari mwaka 2016 katika jiji la Kigali, mjini Huye na Rubavu.

Siku ya Jumanne Kabele ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya michuano hiyo baada ya kuzuru uwanja wa Kimataifa wa Amahoro pia Stade Umuganda na Huye, amedokeza kuwa anaridhishwa na kazi inayoendelea katika viwanja hivyo.

Rais wa Ferwafa Vincent Nzamwita amesema, “ Kabale ametemebelea viwanja vyote vitakavyotumiwa na amekubaliana nasi kuwa maandalizi yanakwenda vizuri kabisa”.

Nzamwita ameongeza kuwa Makandarasi wamemwahidi kuwa kufikia mwezi Septemba mwaka huu, viwanja vyote vitakuwa tayari kwa michuano hiyo na hivyo hakuna kitakachoizua Rwanda kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya CHAN.

CAF itatuma tena wakaguzi wake mwezi Septemba kuona maandalizi yatakapokuwa yamefikia kabla ya droo ya mataifa yatakayoshiriki kufanyika mwezi Novemba.

Michuano ya kufuzu kushiriki katika michuano hii itafanyika kuanzia tarehe 19 mwezi Juni hadi mwisho wa mwezi Agosti ili kupata mataifa 15 yatakayoshiriki katika michuano hiyo.

Amavubi Stars ya Rwanda wao wameshafuzu kwa sababu ni wenyeji na wamepangiwa mchuano wa Kimataifa wa kirafiki tarehe 25 mwezi ujao dhidi ya Afrika Kusini jijini Johannesburg.

Makala ya kwanza ya michuano ya CHAN yalifanyika mwaka 2009 nchini Cote Dvoire na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilikuwa nchi ya kwanza kushinda taji hilo.

Michuano ya mwisho ilifanyika mwaka 2014 nchini Afrika Kusini na Libya wakaibuka mabingwa.

Hayo yakijiri tiimu ya taifa ya soka ya Uganda imeanza mazoezi katika uwanja wa Kimataifa wa Namboole jijini Kampala tayari kwa michuno ya kufuzu katika fainali za mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2017 nchini Gabon.

Kocha Milutin ‘Micho’ Sredojevic ameanza mazoezi hayo na wachezaji 14 kwa maandalizi ya mchuano wa kwanza dhidi ya Bostwana mwishoni mwa juma hili jijini Kampala.

Uganda imepangwa pia katika kundi moja na Burkina Faso na Comoros.

Pamoja na maandalizi hayo, Uganda Cranes pia inajiandaa katika michuano ya kufuzu ya Afrika baina ya wachezaji wa ndani CHAN itakayofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.

Vijana hao wa Micho wamepangiwa kwa mara nyingine kupambana na Tanzania nyumbani na ugenini tarehe 21 mwezi huu kabla ya kurudiana tena mwezi Julai.

Kikosi kinachojiandaa kwa michuano ya CHAN :

Brian Bwete, Mathias Kigonya, Alex Kitata, Kiyemba Ibrahim, Eturude Abel,Ntambi Julius,Katongole Henry, Okello Sylvester, Bukenya Deus, Farouk Musisi, Fahad Muhammed Toko, Mutyaba Muzamil, Paul Mbowa na Frank Kalanda.

Mbali na Uganda mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Kati yanayojiandaa kufuzu michuano hiyo ya CHAN ni pamoja na Djibouti itakayomenyana na Burundi na Ethiopia na Kenya.

Washindi katika hatua hii watafuzu katika mzunguko wa kwanza kujiunga na Sudan ambayo imekwishafuzu.

Rwanda wamefuzu kwa sababu ni wenyeji wa michuano hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.