Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Timu ya Swansea yatafuta kwa udi na uvumba wachezaji wakuipa nguvu ili ifanye vizuri msimu huu

Mchezaji mshambuliaji nyota wa timu ya Uingereza Swansea, Michu, anaeuguza jeraha la mguu toka mwanzoni mwa mwezi novemba, ambae haonekani uwanjani kwa kipindi cha mwezi moja sasa, atafanyiwa upasuaji, na huenda akarudi kuonekana uwanjani kabla ya mwanzoni mwa mwezi wa februari. Hayo yamefahamishwa na kocha wake Michael Laudrup. Kocha huyo ameelezea masikitiko yake, akisema kwamba sio taarifa nzuri kwa timu yake.

Matangazo ya kibiashara

Kukosekana kwa Michu, raia wa Uhispania, mwenye umri wa miaka 27, ni pigo kubwa kwa timu ya Swansea, baada ya mchezaji mwengine wa wingo Nathan Dyer, ambae hashiriki michuano hadi mwezi wa februari kutokana na jeraha la mguu alilolipata wakati Swansea ilipominyana na Norwich.

“Kinachohitajika kwa sasa ni kutafuta wachezaji bora ambao wataziba pengu, ili tuone iwapo tutafanya vizuri”, amesema kocha wa Swansea, kukisalia siku chache michuano ya msimu wa baridi ianze.

Kulingana na taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari vya Uingereza, Swansea huenda ikamuhitaji mshambuliaji wa Liverpool, Iago Aspas, ambae sasa anaichezea timu ya manchester United.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.