Pata taarifa kuu
SOKA-GALATASARAY

Roberto Mancini akabidhiwa mikoba ya kuinoa Galatasaray ya Uturuki kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kukubaliana na Uongozi

Kocha Mkuu wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini amekabidhiwa kibarua cha kuwanoa Mabingwa Watetezi nchini Uturuki Galatasaray iliyomtimua Mkufunzi wake Fatih Terim juma lililopita baada ya kugoma kuongeza mkataba wa muda mrefu.

Kocha Mkuu Mpya wa Klabu ya Galatasaray Roberto Mancini wakati akiifundisha Manchester City
Kocha Mkuu Mpya wa Klabu ya Galatasaray Roberto Mancini wakati akiifundisha Manchester City REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Mancini ameingia mkataba wa kuinoa Galatasaray kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kukubaliana masuala binafsi baina yake na Uongozi wa Klabu hiyo huku ikielezwa amepewa donge nono kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Makubaliano baina ya Uongozi wa Galatasaray na Mancini yalianza tangu mwishoni mwa juma ikiwa ni sehemu ya juhudi za Klabu hiyo kuhakikisha inapata Mkufunzi ambaye anachukua jukumu la kuinoa Klabu hiyo.

Uongozi wa Galatasaray umetoa ahadi ya kumlipa nyongeza ya euro laki tatu iwapo Klabu hiyo itafanikiwa kushinda Taji la Uturuki msimu huu na kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Mancini anatarajiwa kuzoa jumla ya euro milioni tatu nukta tano kwa mwaka na iwapo atafanya vizuri malipo yake yanatarajiwa kuongezeka na kufikia euro milioni nne nukta saba kwa mwaka.

Kocha huyo mpya atakuwa na jukumu la kuhakikisha Galatasaray inarejesha makali yake kwenye Ligi Kuu nchini Uturuki baada ya kuanza vibaya msimu huu na kufuatiwa na kupoteza mchezo dhidi ya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Galatasaray ipo pointi nane nyuma ya vinara wa Ligi Kuu Nchini Uturuki Fenerbahce kutokana na kushinda mchezo mmoja tu pekee miongoni mwa michezo yao mitano ya msimu huu.

Mancini amekuwa na rekodi nzuri wakati akiifundisha Manchester City kutokana na kufanikiwa kuipa taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 35 huku pia akishinda Kombe la Chama Cha Soka FA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.