Pata taarifa kuu
SOKA-ULAYA

Bayern Munich watwaa ubingwa ligi ya mabingwa barani Ulaya

Klabu ya soka ya Bayern Munich imetwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu baada ya kupata bao la ushindi dhidi ya Borussia Dortmund katika mchuano wa fainali uliopigwa usiku wa kuamkia jumapili ndani ya dimba la Wembley jijini London nchini Uingereza.

REUTERS/Stefan Wermuth
Matangazo ya kibiashara

Bao la ushindi lilipachikwa kimiani na mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Arjen Robben katika dakika ya 89 ambaye aliibuka furaha za mashabiki wa Munich ambao wameshuhudia timu yao ikicheza fainali tatu mfululizo bila kupata ushindi.

Mchunao huo ulimalizika kwa mabao 2 ya Munich dhidi ya lile moja la Dortmund lililopachikwa na Gundogan aliyesawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 67 ya mchezo huo.

Bayern wametwaa ubingwa baada ya kuizamisha Juventus kwenye hatua ya robo fainali pamoja na Barcelona katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Kocha anayeondoka klabuni hapo Jupp Heynckes ameeleza kufurahishwa na wachezaji wake waliompa heshima katika mchuano wake wa mwisho wa ligi ya mabingwa akiwa klabuni hapo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.