Pata taarifa kuu
FIFA-SEPP BLATTER

Sepp Blater kuwania tena urais FIFA baada ya kumaliza muda wake 2015

Rais wa shirikisho la soka duniani, FIFA Sepp Blatter amesema kuwa ana mpango wa kuendelea kuongoza shirikisho hilo kwa miaka mingine minne baada ya muda wake kukamilika mwaka 2015.

REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wajumbe wa shirikisho la soka barani Asia, AFC nchini Malaysia Blatter mwenye umri wa miaka 77 hata hivyo amesema kuwa atajiuzulu baada ya muda wake kumaliza lakini kuna uwezekano akaendelea kuongoza.
 

Aidha, rais huyo wa soka dunaini amesema kuwa huu hautakuwa muda wake wa mwisho kuongoza bali wa kushinikiza mabadililko katika shirikisho hilo.
 

Blatter ameopngeza kuwa mabadiliko muhimu katika ngazi ya uongozi yamesaidia pakubwa mno kukbailiana na ufisadi katika shirikisho hilo na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
 

Mbali na hayo, Blatter amesisitiza kuwa wakati umefika kwa shirikisho la soka barani Asia kupewa nafasi zaidi katika mashindano ya kombe la dunia ili kuwe na usawa katika mabara yote.
 

Michel Platini, rais wa shirkisho la soka barani Ulaya, UEFA amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kumrithi Blatter anashutumiwa na uongozi wa sasa wa FIFA kwa kutumia mamlaka yake vibaya katika uongozi wake wa soka barani Ulaya.
 

Siku ya Alhamisi,wajumbe wa soka barani Asia walimchagua Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa kutoka Bahrain kama kiongozi mpya wa shirikisho hilo la soka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.