Pata taarifa kuu
SOKA

Nahodha wa zamani wa timu ya Uingereza Michel Owen atangaza kustaafu kucheza soka

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Uingereza Michael Owen ametangaza kuwa atajiuzulu kucheza soka mwisho wa msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Owen mwenye umri wa miaka 33 aliichezea Uingereza mara 89 na kuifungia mabao 40 kati ya mwaka 1998 na 2008 alipoacha kuichezea timu ya taifa.

Mbali na Uingereza Owen aliwahi kuichezea klabu ya Liverpool kati ya mwaka 1996 na 2004 na kuifungia mabao 158 kwa kuicheza mara 297.

Vlabu vingine alivyochezea ni pamoja na Real Madrid ya Uhispania, Newscatle , Manchester United na Stoke City zote za Uingereza.

Owen atakumbukwa kama mchezaji aliyefunga mabao 220 wakati akicheza soka ya kulipwa katika vlabu mbalimbali na mwaka 2001 alitajwa kuwa mchezaji bora barani Ulaya mwaka 2001.

Mchezaji huyo amesema kuwa wakati wa kuacha kucheza soka umefika na anaamini kuwa baada ya kuliwakilisha taifa lake na klabu aliyochezea wakati wake wa kupumzika umefika.

Aidha, Owen amewashukuru wachezaji wenzake, Makocha na viongozi wengine wa vlabu mbalimbali na timu ya Uingereza kwa kumsaidia kufika kileleni mwa uchezaji wake wa soka.

Kwa sasa Owen anaichezea klabu ya Stoke City ambayo ameifungia bao moja baada ya kuicheza mechi saba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.