Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Manchester City yatangaza nia yake ya kumuuza Mshambuliaji wake Balotelli kwenda Italia

Klabu ya Manchester City imeanzisha mazungumzo na Timu za AC Milan na Juventus juu ya kutaka kumuuza mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia anayekipiga katika klabu hiyo Mario Bolotelli kama watakuwa tayari kufikia makubaliano.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia anayekipiga katika Klabu ya Manchetser City Mario Balotelli
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia anayekipiga katika Klabu ya Manchetser City Mario Balotelli
Matangazo ya kibiashara

Manchester City imetangaza kitita cha euro milioni 24 kwa ajili ya kumuuza Balotelli na huenda thamani yake ikaongezeka kulingana na mafanikio ambayo atayapata katika Klabu itakayomnasa huko Serie A.

Mabingwa hao watetezi nchini Uingereza wamefikia uamuzi huo wa kumuuza Balotelli kutokana na kuanza kuchoshwa na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu ambavyo amekuwa akivionesha mara kwa mara.

Balotelli mshambuliaji mwenye vituko vingi amekuwa mara kadhaa akiingia kwenye malumbano na wachezaji wenzake lakini tukio la hivi karibuni ni lile la kulumbana na Kocha wake Roberto Mancini.

Licha ya uwepo wa uvumi wa kuuzwa kwa Balotelli lakini mshambuliaji huyo amejumuishwa kwenye kikosi cha Manchester City kitakachoshuka dimbani kukabiliana na QPR jumanne hii.

Kocha Msaidizi wa Manchester City David Platt aliwashangaza waandishi wa habari baada ya kukanusha uvumi huo na kusema Balotelli hatouzwa mwezi huu wa januari kueleka AC Milan.

Platt amesema ni vugumu kwa sasa kuuza mchezji kutokana na Klabu hiyo kukabiliwa na upungufu wa wachezaji kwa kuwa kuna wachezaji ambao wanatumikia Timu za Taifa na wengine majeruhi.

Balotelli amefunga goli moja pekee katika michezo kumi na nne ambayo amecheza kitu ambacho kinadhihirisha kiwango chake msimu huu kimeshuka tofauti na ambavyo amecheza msimu uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.