Pata taarifa kuu
Cote D' Ivoire

Cote D'Ivoire yaendelea kuongoza kwa ubora Afrika katika soka

Shikisho la soka duniani, FIFA limetoa orodha ya mataifa bora duniani kwa kipindi cha mwezi wa Desemba mwaka uliopita,huku mataifa ya Afrika yakiangaziwa mno kabla ya kuanza kwa michuano ya kuwania taji la Afrika siku ya Jumamosi.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Cote D' Ivoire inaongoza kwa mara nyingine kama timu bora barani Afrika ikifuatwa na Algeria ambayo ni ya nafasi ya pili huku Mali ikifunga orodha ya timu tatu bora barani Afrika.

Katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati Uganda bado inaongoza ikifuatwa na Burundi , DR Congo ,Tanzania ,Kenya na Rwada.

Kwingineko huku ikisalia siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya kuwani taji la kombe mataifa ya Afrika ,timu mbalimbali zimetamatisha maandalizi yake huku kibarua cha kwanza kikiwa kati ya wenyeji Bafana Bafana na Cape Verde.

Kocha wa Bafana Bafana Gordon Igesud amesema kuwa bado anakiweka siri kikosi cha wachezaji 11 kitachoanza katika mchuano wa ufunguzi siku ya Jumamosi muda mchache kabla ya kuanza kwa mchuano huo.

Naye Kocha wa Chipolopolo ya Zambia Harve Renard amesema kuwa hawezi kutamba kuwa vijana wake watanyakua tena taji hilo kwa kile alichokisleza kuwa kuna timu nzuri kama Ghana na Cote Dvoire ambazo pia amezipa nafasi kubwa ya kushinda taji hizo.

Zambia ndio mabingwa watetezi wa taji hili kombe walilonyakua mwaka uliopita wakati wa mahindano haya huko Gabon na Equitorial Guinea.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.