Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha wa Manchester City Mancini bado anampango wa kusajili kipindi cha dirisha dogo

Kocha Mkuu wa Manchester United Roberto Mancini ameonesha utayari wake wa kusajili wachezaji zaidi katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambalo limefunguliwa mwezi huu wa january lengo ni kuimarisha kikosi chake.

Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini aeleza mpango wa kusajili wachezaji wakati wa dirisha dogo
Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini aeleza mpango wa kusajili wachezaji wakati wa dirisha dogo
Matangazo ya kibiashara

Mancini amesema atalazimika kuingia sokoni mwezi january kutokana na kuwakosa wachezaji kutokana na majeraha huku wengine watatu wakikosekana mwezi huu kutokana na kuhitajika kutumia mataifa yao.

Mancini ametangaza hatua hiyo kutokana na kutarajiwa kuwakosa wachezaji watatu wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast ambao watakuwa kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON.

Kukosekana kwa Yaya Toure, Kolo Toure na Abdul Razak ambao wote watakuwa kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo yatafanyika nchini Afrika Kusini kuanzia mwezi januari hadi februari.

Mancini anaonekana kukutwa na kiwewe kipindi hiki ambacho anamkosa beki wake Micah Richards ambaye anakabiliwa na majeruhi na huenda akarejea kwenye kikso mwishoni mwa mwezi wa februari.

Manchester City inaendelea kukabiliwa na majeruhi kadhaa wakiwemo Jack Rodwell Maicon, Mario Balotelli na Aleksandar Kolarov ambao wote hawajulikani watarudi lini hatua ambayo inamfanya Mancini kuhisi anastahili kusajili zaidi.

Mancini amekataa mpango wa kuuza wachezaji akidai kikosi chake kina wachezaji wachache na badala yake anataka kuimarisha kikosi chake na kuendelea kutetea ubingwa wake kwenye msimu huu.

Kocha Msaidizi wa Manchester City David Platt juma lililopita amekiri kushangazwa na uwepo wa mpango wa klabu hiyo kusajili katika mwezi januari kutokana na kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.