Klabu ya Arsenal yafuzu hatua ya mtoano klabu bora Ulaya
Klabu ya soka ya Uingereza Arsenal imefuzu katika hatua ya mwondoano kuwania taji la klabu bora barani Ulaya baada ya kuifunga Montpellier ya Ufaransa mabao 2 kwa bila katika uwanja wa Emirates.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mabao ya Arsenal yalitiwa kimyani katika kipindi cha pili na Jack Wilshere katika dakika ya 49 na Lukas Podolski katika dakika ya 63 ya mchezo huo.
Nayo Manchester City pia ya Uingereza imeondolewa katika kianyanganyiro hicho baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja na Real Madrid ya Uhsipania katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad.
Manchster City ambao ni mabingwa wa ligi nchini Uingereza walihitaji ushindi jana usiku lakini bao la mapema la Karim Benzema liliwaharibia mahesabu ya kusonga mbele.
Sergio Aguero aliiwaazishia Manchester City kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa vibaya Alvaro Arbeloa.
Katika matokeo mengine,Paris Sinat Gemain waliwashinda Dynamo Kiev mabao 2 kwa 0 huku Borrusia Dortmund ikiichabanga Ajax FC kwa mabao 4 kwa 1.