Pata taarifa kuu
michezo

Kiungo wa pembeni wa zamani wa manchester united Kenny Morgans afariki dunia

Kiungo wa pembeni wa zamani wa manchester united Kenny Morgans ambaye alinusurika katika ajali ya ndege ya mwaka 1958 amefariki dunia mwishoni mwa juma baada ya kuugua na kufikishwa hospitali siku ya jumamosi.

Mchezaji wa zamani wa Man united Kenny Morgans aliyefariki mwishoni mwa juma
Mchezaji wa zamani wa Man united Kenny Morgans aliyefariki mwishoni mwa juma bbc.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mtandao wa klabu ya Manchester United Morgans alifikishwa hospitali jumamosi kupatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambapo baada ya muda mfupi aliaga dunia.

Morgan akiwa na umri wa miaka 18 aliichezea Man united mechi yake ya kwanza dhidi ya Leicester City mnamo tarehe 21 December 1957.

Morgan ni majeruhi aliyenusurika katika ajali ya ndege iliyobeba timu hiyo ikitokea kushiriki kombe la ulaya ambapo ndege ilipata ajali tarehe 6 february na kusababisha vifo vya watu 23.

Kama bahati Morgans aliokolewa na waandishi wa habari wawili raia wa Ujerumani.

Aliweza kuendelea na uchezaji wa mpira ambapo alijiunga na Swansea city akitokea Old Trafford mwaka 1961 ambapo alistaafu mchezo huo mwaka 1967.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.