Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Mancini akiri alikuwa na mpango wa kuihama Manchester City msimu uliopita kabla hajaongeza mkataba

Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini amekiri alikuwa na mpango wa kuikacha Klabu yake mwishoni mwa msimu iliyopita kabla hajafikia uamuzi wa kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia kwa miaka mitano.

Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini ambaye amesema alipanga kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita
Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini ambaye amesema alipanga kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita
Matangazo ya kibiashara

Mancini amewaambia wanahabari alikuwa na fursa kubwa ya kuhama manchester City kutokana na klabu kadhaa kuonekana kusaka sahihi yake lakini mpango huo ulionekana kukwama.

Kocha huyo ambaye alifanikisha kuwapa Ubingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza Manchester City msimu uliopita ameweka wazi kulikuwa na klabu nane ambazo zilikuwa zinamwania lakini hakuwa tayari kuondoka.

Mancini alilazimika kutoa maelezo baada ya waandishi wa habari kuumuliza kama kweli alikuwa anataka kujiunga na klabu ya Monaco mwishoni mwa msimu uliopita na yeye akasema alikuwa wanawaniwa na klabu nane zaidi.

Kocha huyo ameweka bayana kwa sasa ana furaha sana kuendelea kusalia Manchestr City na kuhakikisha anaijenga timu hiyo ili iweze kuendeleza ushindani na hatimaye kutetea Kombe la Ligi walillotwaa msimu uliopita.

Mancini amesema ameongeza mkataba na Manchester City kwa kuwa ana imani na kikosi aliachonacho kitafanya mambo makubwa na kutwaa mataji na kuwataka mashabiki kuwa wavumilivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.