Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA kimeanzisha uchunguzi wa madai ya kutolewa kwa maneno ya kibaguzi na Mwamuzi Clattenburg

Chama Cha Soka nchini Uingereza FA kimeanzisha uchunguzi dhidi ya mwamuzi Mark Clattenburg ambaye anatuhumiwa na Klabu ya Chelsea kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya John Obi Mikel na Juan Mata.

Mwamuzi Mark Clattenburg akiwa na Mchezaji wa Chelsea John Mikel Obi na hapa ndiyo anatuhumiwa kutoa maneno ya kibaguzi
Mwamuzi Mark Clattenburg akiwa na Mchezaji wa Chelsea John Mikel Obi na hapa ndiyo anatuhumiwa kutoa maneno ya kibaguzi
Matangazo ya kibiashara

Chama Cha Soka FA kimeamua kuanzisha uchunguzi huo baada ya Chelsea kuwasilisha rasmi madai hayo wakimtuhumu Clattenburg kutoa maneno ya kibaguzi katika mchezo wa jumapili uliopigwa kwenye Dimba la Stamford Bridge.

Chelsea ambao walikubali kichapo cha kwanza cha nyumbani kutoka kwa Manchester United cha magoli 3-2 katika kipindi cha miaka kumi wameonekana kutoridhishwa hata na maamuzi wa Clattenburg.

Chama Cha Soka nchini Uingereza FA kimethibitisha kupitia taarifa yake kuanza uchunguzi huo wa kutolewa kwa maneno ya kibaguzi lakini hawakatoa maelezo ya zaidi uchunguzi huo utachukua muda gani na adhabu inaweza ikawa ipi iwapo akibainika.

Chama Cha Soka FA kutokana na kuanza kufanya uchunguzi ya madai hayo ya kibaguzi ambayo yanamkabili Clattenburg wamefikia uamuzi wa kutompangia mchezo wowote mwishoni mwa juma hili.

Tayari Chama Cha Waamuzi wa Kulipwa PGMO kimeeleza kwenye taarifa yake wanafanyika kazi madai ambayo yametolewa na Chelsea dhidi ya Clattenburg ili kubaini kama kweli alitenda kosa hilo.

Naye Mwanasheria wa Chama Cha Wachezaji Weusi Peter Herbet kwenye taarifa yake ameituhumu Polisi kwa kushindwa kuchukua hatua kutokana na tuhuma zao kuweka bayana wachezaji ambao wamekumbana na maneno hayo ya kibaguzi ni Juan Mata na John Mikel Obi.

Mapema mwamuzi wa zamani wa Uingereza Graham Poll alisema wale ambao wanaweza kutoa ushahidi ni waamuzi wasaidizi ambao huwa wanasikia kila kitu kinachotamkwa na mwamuzi kupitia vifaa maalum ambavyo huwa wanavaa.

Mark Clattenburg aliingia kwenye lwama kutokana na kutoa kadi nyekundu mbili kwa wachezaji wa Chelsea ambao ni Branislav Ivanovic na Fernando Torres huku akikubali goli la Javier Harnandez ambalo linatajwa lilifungwa akiwa kwenye eneo alilozidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.