Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers asikitishwa na uamuzi wa mwamuzi kumpa kadi nyekundu mchezaji wake

Kocha wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amekiri timu yake kucheza chini ya kiwango na kuongeza kuwa ilikuwa bahati kwa timu yake kuibuka na ushindi kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.

Jonjo Shelvey akioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi, Mark Halsey
Jonjo Shelvey akioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi, Mark Halsey Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ambao ulikuwa ni kama wa wapinzani wa jadi umeshuhudiwa na maelfu ya mashabiki huku timu hizo mbili zikitumia mchezo huo kuwakumbuka mashabiki ambao walipoteza maisha wakati wa tukio la Hilsbrough.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Ferguson amesema kuwa kiwango cha timu yake kilikuwa duni na kama sio kukosa umakini wa washambuliaji wa Liverpool basi wangefungwa kwenye mchezo wao.

Kwenye mchezo huo Liverpool ndi waliokuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa nahodha wao Steven Gerald kabla ya beki Rafael na mshambuliaji Robin Van Persie hawajaipatia timu yao magoli ya ushindi.

Mchezo mwingine uliwakutanisha timu ya Manchester City waliokuwa wenyeji wa klabu ya Arsenal kwenye mchezo ambao umeshuhudia timu hizo zikitoka sare ya goli moja kwa moja.

Mechi nyingine Newcastle wakiwa nyumbani walichomoza na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Norwich wakati Tottenham wakiwa nyumbani wakichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya QPR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.