Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Klabu za Manchester United na Liverpool zinamatumaini Suarez na Evra watashikana mikono kwenye mchezo wa Jumapili

Klabu za Manchester United na Liverpool zinamatumaini wachezaji wao Patrice Evra na mwenzake Luis Suarez watapeana mikono kabla ya mchezo baina ya mahasimu hao wawili ambao utapigwa jumapili kwenye dimba la Anfield.

Mshambulizji wa Klabu ya Liverpool Luis Suarez akikataa kupeana mkono na Beki wa Manchester United Patrice Evra
Mshambulizji wa Klabu ya Liverpool Luis Suarez akikataa kupeana mkono na Beki wa Manchester United Patrice Evra
Matangazo ya kibiashara

Maofisa kutoka klabu hizo wamesema wanaimani tofauti baina ya wachezaji hao wawili zitazikwa rasmi baada ya Suarez kukutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi Evra na hivyo kufungiwa na Chama Cha Soka FA.

Viongozi hao wa Klabu hizo kubwa nchini Uingereza wapo kwenye mazungumzo ya kumaliza tofauti walizonazo ili kuhakikisha wanaendeleza umoja baina yao licha ya kuendelea kuwa wapizani uwanjani.

Tukio la ubaguzi ambalo alilifanya Suarez dhidi ya Evra lilisababisha mchezaji huyo kufungiwa michezo minane kitu ambacho kilichochea uhasama mkubwa baina ya Manchester na Liverpool.

Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameshaweka bayana utayari wao kuiunga mkono Liverpool kwa njia zote ambazo zinawezekana akirejea tukio la mwaka 1989 lililoshuhudia vifo vya watu tisini na sita.

Manahodha wa klabu hizo Steven Gerrard na Nemanja Vidic wanatarajiwa kabla ya kuanza kwa mchezo huo kurusha hewani maputo tisini na sita ikiwa ni ishahara ya kumbukumbu ya mashabiki hao waliopoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.