Pata taarifa kuu
Kombe la Uingereza

Manchester United yalazimishwa sare ya mabao 4-4 na Everton

Everton yailazimisha Manchester United sare ya mabao 4-4 katika mpambano wa kusisimua hasa dakika za mwisho kwenye uwanja wa Old Trafford. Matukio hayo yanaweka hatihati matumaini ya Manchester United kunyakua taji la ubingwa la ligi kuu ya Uingereza

wachezaji wa Manchester United
wachezaji wa Manchester United REUTERS/Russell Cheyne
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji machachari wa Man United Wayne Rooney aliisawazishia Manchester United baada ya kuunganisha kwa kichwa pasi kutoka kwa Nani baada ya bao la kuongoza la Everton lililofungwa kwa na Nikica Jelavi.
 

Danny Welbeck na Nani waliipatia Manchester United mabao mawili kabla Marouane Fellaini kufunga bao moja jingine kwa Everton. Rooney alionekana kuipatia ushindi Man United alipopachika bao la nne na muda mfupi baadae Everton wakacharuka na kupachika mabao mawili katika muda wa dakika tatu kupitia kwa Jelavic na Steven Pienaar.

Katika dakika za mwisho, Patrice Evra alipiga mpira wa kichwa uliogonga mlingoti wa lango la Everton akiwa karibu kabisa na baadae mlinda mlango wa Everton Tim Howard aliokoa kwa ustadi mkubwa mkwaju wa Rio Ferdinand na kuinyima ushindi Manchester United. Manchester United hata hivyo bado wanaongoza Ligi Kuu ya England wakiwa na pointi 83.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.