Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Man Utd yaendelea kung'ang'ania kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza

Ligi kuu ya nchini Uingereza imeendelea kushika kasi na sasa kinyang'anyiro kimebaki kwa timu mbili za Manchester City na Manchester United kuwania ubingwa wa ligi ya Uingereza.

Mchezaji wa Man Utd Ashley Young akianguka ndani ya eneo la hatari, penalty ambayo ilizua utata
Mchezaji wa Man Utd Ashley Young akianguka ndani ya eneo la hatari, penalty ambayo ilizua utata Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana kulikuwa na mchezo mmoja wa ligi hiyo ambapo mashetani wekundu Man Utd waliwakaribisha Aston villa kwenye mchezo ambao umeshuhudia Man Utd wakiondoka na ushindi wa mabao 4-0.

Kwenye mchezo huo ambao pia ulikuwa wa upinzani mkali, ulishuhudia Man utd waiandika bao lao la kwanza kupita kwa Wyne Rooney aliyefunga kwa njia ya penalty baada ya Ashley Young kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Man utd walifanikiwa kuandika bao la pili kuptia kwa Danny Welback aliyeunganisha vema pasi ya Patrice Evra, kabla ya Rooney na Luis Nani kuiandikia timu yao bao la tatu na la nne.

Manchester City yenyewe ikiwa ugenini ilicheza na Norwich City na kufanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabo 6-1 huku Carlos Tevez akiifungia timu yake mabo 3 kati ya sita.

Kwenye mechi zingine za Jumamosi, West Brownich walichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya QPR, wakati Swansea wakichomoza na ushindi wa mabo 3-0 dhidi ya Blackburn huku Sunerland na Wolvhampton wakitoka suluhu ya bila kufungana.

Kwa matokeo hayo ni wazi ushindani ni mkali kileleni mwa ligi hiyo ambapo, Man Utd inaongoza ikiwa na alama 82 wakati Man City ni ya pili ikiwa na alama 77 ikiwa wanatofauti ya alama 5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.