Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Roberto Mancini awataka wachezaji kupima afya mara mbili kwa mwaka

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema wachezaji wa Ligi Kuu hawana budi wapimwe afya zao mara mbili kwa mwaka. 

Kikosi cha wachezaji wa Manchester city wakishangialia ushindi
Kikosi cha wachezaji wa Manchester city wakishangialia ushindi REUTERS/Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Mancini ametoa maoni yake baada ya Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu Richard Scudamore kusema kutakuwa na utaratibu wa kupitia masuala ya upimaji baada ya Fabrice Muamba kuanguka na kuzirai kutokana na matatizo ya moyo.

Watu wa huduma ya kwanza walitumia dakika sita wakijaribu kuamsha mapigo yake ya moyo baada ya kiungo huyo wa Bolton kupoteza fahamu walipocheza na Tottenham Hotspur siku ya Jumamosi.

Kiwango cha uangalizi alichopatiwa kimesaidiwa sana kutokana na mabadiliko yaliyowekwa na Ligi Kuu baada ya mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech kuvunjika fuvu la kichwa mwaka 2006.

Meneja wa Manchester City Mancini amesisitiza utaratibu wa matibabu nchini England bado haufanani na wa Italia.

Naye Meneja wa Liverpool Kenny Dalglish alisema kwa upande wake anaridhika na kiwango cha muda ambacho wachezaji wanafanyiwa uchunguzi wa afya zao.

"Wachezaji wetu wanachunguzwa afya zao kila baada ya miaka miwili," alisema Dalglish. "Baadhi wanakuja katika klabu kwa uhamisho au kijana wa miaka 17 anafanyiwa uchunguzi mara moja.

Muamba alikimbizwa haraka katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu katika hospitali inayotibu maradhi ya moyo ya London Chest baada ya kupatiwa huduma ya kwanza kufuatia kuanguka na kupoteza fahamu katika dakika ya 42 ya mchezo kuwania Kombe la FA hatua ya robo fainali .

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.