Pata taarifa kuu
Uingereza

Manchester City kusaka uongozi wa ligi

Manchster City wanacheza ugenini dhidi ya Stoke City Jumamosi hii katika mchuano wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kutafuta ushindi wa kuwawezesha kurejea kileleni mwa ligi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Mancshester City katika uwanja wa Britannia utawawezesha kuwa mbele ya viongozi wa ligi hiyo Manchester United ambao wana alama 70.

Manchsters United hawatakuwa na mechi mwishoni mwa juma hili hadi siku ya Jumatatu watakapokuwa wenyeji wa Fulham katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford.

Katika mechi zingine zinazochezwa Jumamosi hii Chelsea watavaana na Tottenham Hotspurs,Arsenal watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates dhidi ya Aston Villa wakati Liverpool wakiwa nyumbani kwao Anfield kumaliza kazi na Wigan Athletic.

Hata hivyo,macho yote yatakuwa yaangaziwa katika mchuano kati ya Bolton Wanderes na Blackburn, mchuano wa kwanza kwa Bolton tangu kiungo wao wa kati Fabrice Muamba alipolazwa katika hospitali ya moyo jijini London mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuzirai uwanjani.

Kwingineko,Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya Liverpool Iain Ayre amesema Luis Suarez ataongezewa mkataba katika klabu hiyo ili kumzuia mchezaji huyo kuondoka kutokana na madai kuwa alikuwa anatafutwa na klabu ya Ufaransa ya Paris Saint Germain.

Suarez mwenye umri wa miaka 25 raia wa Uruaguay alitia saiani mkataba wa kuichezea Liverpool miaka 5 alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.