Pata taarifa kuu
Ligi kuu ya Uingereza

Arsenal kupambana na Udinese

Kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Kocha wake Arsene Wenger kitakuwa na kibarua kigumu hii leo cha kusaka nafasi ya kutinga katika hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya watakapokipiga na Udinese kwenye mchezo wao wa pili.

Les trois joueurs d'Arsenal : Sagna, Clichy et Nasri (de gauche Γ  droite).
Les trois joueurs d'Arsenal : Sagna, Clichy et Nasri (de gauche Γ  droite). Reuters
Matangazo ya kibiashara

Arsenal wanaenda kuwavaa Udinese wakiwa hawana wachezaji wao mahiri mawili ambao ni Samir Nasri ambaye anakamilisha usajili wake kujiunga na Manchester City wakati Jack Wilshere yeye anasumbuliwa na majeruhi.

Kikosi cha mzee Wenger kinashuka dimbani kikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi finyu kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Udinese ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Emirate na sasa huu ndiyo mchezo utakaoamua nani wa kusonga mbele.

Katika hatua nyingine Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kupata tiketi ya kushiriki hatua ya makundi baada ya kuwafunga FC Zurich na kuungana na Villarreal iliyowaangusha Odense BK wakati Dinamo Zagreb nayo haikutaka kubaki nyuma.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.